WADAU wa vita dhidi ya UKIMWI wilaya ya Ikungi,wametakiwa kutobweteka na
kitendo cha kupungua kwa maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI,na
badala yake waongeze juhudi zaidi ili ifikapo mwaka 2015,maambukizi ya
virusi vya UKIMWI,unyanyapaa na vifo vinavyosababishwa na UKIMWI,vifikie
asilimia sifuri.
Changamoto hiyo imetolewa juzi na afisa
ustawi wa jamii sekretarieti ya mkoa wa Singida,Zuhura Kyara,wakati
akifungua mkutano wa wadau wa UKIMWI wilaya mpya ya Ikungi uliofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini hapa.
Alisema
maambukizi mapya ya VVU katika halmashauri ya wilaya ya Singida na
Ikungi,takwimu zinaonyesha kuwa yamepungua kutoka asilimia nne hadi
mbili hadi mwaka huu.
Kyara alisema hayo ni mafanikio mazuri lakini hata hivyo,juhudi zaidi
zinapaswa kuongezwa ili kufikia mwaka 2015,pasiwepo kabisa na maambukizi
mapya,unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI kama dunia ilivyoazimia.
"Dira
na maono yetu kama wadau,ni kuhakikisha tunaweka misingi imara yenye
mwelekeo wa kutimiza azma hii.Hivyo tutumie fursa hii ya mkutano huu
kufanya majadiliano juu ya mikakati ya kukabili changamoto mbalimbali
za
VVU/UKIMWI",alifafanua Karya.
Afisa huyo alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kupunguza
maambukizi yanayosababishwa na ngono hasa kwa vijana wanaofanya ngono
kama sehemu ya kujipatia kipato.
Karya
alitaja changamoto zingine kuwa ni kupunguza vifo vyote
vinavyosababishwa na ugonjwa wa kifua
kikuu na kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wote
wanaoishi na VVU na kupatiwa matibabu yote wanayostahili kupewa.
MWISHO.
Post a Comment