KAULI YA ISMAIL JUSSA

Picture
Kwa mara nyengine tena leo hii kumetangazwa kutokea tukio la kumwagiwa acid ambapo imeelezwa jioni hii Padri Joseph Magamba amemwagiwa acid maeneo ya Sunshine Internet Cafe hapo Mlandege, mjini Zanzibar. Binafsi nalaani vikali kitendo hicho cha kinyama na cha kishenzi kabisa.
Picture
Juzi tu Jumatano nilisoma katika gazeti la Mwananchi tukio la mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi Christian Msema wa Mburahati, Dar es Salaam kumwagiwa acid na watu wasiojulikana waliokuwamo kwenye bajaj.

Matukio haya ni ya kinyama na ya kutisha na yanaonekana kushika kasi kila uchao. Bahati mbaya licha ya
 Polisi kutangaza operesheni maalum ya kutafuta kile walichokiita mtandao wa acid hakuonekani mafanikio yoyote.

Hivi uwezo wa uchunguzi wa Jeshi la Polisi umeshuka kiasi hichi? Na kwa nini hadi leo Serikali haijapiga marufuku uuzaji au upatikanaji mwengine wa acid ambao unaonekana kufanyika kiholela kiasi cha kupatikana kirahisi na kutumika kufanyia uhalifu kiasi hichi?

Yeyote au kikundi chochote kilicho nyuma ya matukio haya kinapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kusakwa ili kuchukuliwa hatua kali dhidi yao.

Ismail Jussa
Muwakilishi – Mji Mkongwe

KAULI YA Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar (VUK) 


Kwa mara nyengine tena tukio la kinyama na la aibu limetokea kwa matumizi ya tindi kali dhidi ya binaadamu ambapo leo hii Kiongozi wa Kidini akiwa ni Padri Joseph Mwang'amba, alieshambuliwa akiwa maeneo ya Mkamasini, Mjini Unguja.

Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar (VUK) lina laani tukio hilo kwa nguvu zote na hakuna sababu yoyote ile ya kutumia tindi kali kama silaha dhidi ya binaadamu.

VUK inasikitishwa na matendo kama haya ambayo yanazidi kujenga uadui baina ya Wazanzibari ambapo huu ni wakati wa Wazanzibari kuwa pamoja zaidi na wazuie vishawishi vyovyote vya kuwagawa.

Kama ambavyo inalaani matumizi kwa binadaamu yoyote pia inalaani matumizi ya tindi kali dhidi ya viongozi wa kidini na inasimama kuwa hakuna sababu yoyote ile ya kufanya hivyo ama kwa njia ya kisasi, mgogoro kwa sababu njia za amani hazijafungwa na kwa hakika zimezoeleka kutumika na Wazanzibari.

VUK inawataka wananchi kushikamana, lakini hasa vijana wasikubali kuingizwa katika matukio kama hayo lakini pia wasishabikie na zaidi wasiwafiche waovu kama hawa kwa kuwatolea ripoti kwa mamlaka za ulinzi na usalama.

VUK inawataka wananchi kujua matukio kama haya sio tu ya hatari, lakini pia wanachafua jina na amani ya nchi na kwa hivyo wakati huu ndio muwafaka kwa kila mwananchi kuwa macho na kuwa mlinzi wa watu ambao wanataka kuiharibia sifa na jina jina la Zanzibar.

VUK inalitaka Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa itoe majibu ya matukio kama haya ambayo sasa yanachafua akhlaki na utengamano wa Wazanzibari, na majibu hayo tunayataka leo kabla ya kesho maana kuanzia kesi ya Sheikh Fadhil Soraga, Sheha wa Tomondo na pia vijana wawili wa Kiingereza ambao ni Katie Gee (18) na Kirstie Trup (18).

VUK inavitaka vyombo hivyo virudishe imani ya Wazanzibari ambao wamezoea jamii inayoishi kwa kupendana na kusaidiana na ambapo sasa inafisidika kwa kuchukina na unyama.

Pia VUK inatoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutumia kila aina ya uwezo iliyonayo, na kwa umma kuona uwezo huo unatumika, kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua.

Vilevile SMZ ihakikishe inadhibiti upatikanaji na usambazaji wa tindi kali, ambayo hivi sasa inaonekana kupatikana kwake ni rahisi na matumizi yake ni hatari kwa umma.

Kila mtu ajue na aone kuwa anaweza kuwa hatarini kushambuliwa kwa silaha hii na hivyo wajibu wa kuchukia na kuchukua hatua ni wa kila mtu lakini hasa vijana ambao wao huwapo mitaani saa zote.

VUK ina mpa pole Padri Joseph Magamba na inamuombea Mungu ampe afueni ya haraka na tunaungana na jamaa na waumini wake katika kipindi hiki kigumu.

Salum Abdallah Salum
Kaimu Mwenyekiti
0713742255

Chanzo na tovuti ya www.wavuti.com































































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.