MCHEZAJI MPYA wa Manchester United Marouane Fellaini amesema anataka kumuiga Gwiji wa Mabingwa hao Roy Keane.

KEANO
Leo Fellaini, mwenye Miaka 25, anatarajiwa kucheza Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Man United dhidi ya Crystal Palace Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

Jana, wakati akitambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya baada ya kununuliwa kwa Pauni Milioni 27.5 kutoka Everton, Fellaini alitamka: “Meneja ndie ataamua wapi nicheze lakini nataka nicheze kama Kiungo Mkabaji. Keane alikuwa Mchezaji mwenye ari na mpiganaji mwenye uwezo wa kunyang’anya Mpira wowote. Pengine na mimi naweza kufanya hivyo. Naweza kunyang’anya Mpira, kuokoa na naweza kucheza bila rafu.”

Roy Keane alikuwa Mchezaji wa Kimataifa wa Republic of Ireland ambako alikuwa Nahodha wa Timu hiyo pamoja na Manchester United ambako alicheza Old Trafford toka Mwaka 1993 hadi 2005 na ndie alikuwa nguzo ya Wachezaji walioiwezesha Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Ligi mara 7 katika kipindi hicho.

Pia Keane, ambae sasa ana Miaka 42, aliisaidia Timu ya Sir Alex Ferguson kutwaa Ubingwa wa Ulaya mara moja, FA CUP 4, Ngao ya Jamii 4 na Ubingwa wa Dunia mara moja.
Akiwa na Everton, chini ya David Moyes alipokuwa huko, Fellaini mara nyingi alikuwa akichezeshwa Kiungo wa kushambulia lakini sasa Fellaini anataka arudi nyuma na kuwa KiungoFLETCHERMkabaji.
Wakati huo huo, Moyes amethibitisha kuanza tena Mazoezi kwa Kiungo Darren Fletcher ambae alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa sugu wa tumbo uliomfanya acheze Mechi 7 tu katika Miaka miwili.

Juzi Alhamisi Fletcher alianza Mazoezi na Moyes amesema watamjenga pole pole hasa kuhakikisha anaongeza uzito ambao amepungua sana.

Pia Moyes alisema watamfanyia tathmini Straika wao Wayne Rooney kuangalia uwezekano wa yeye kucheza Mechi ya leo na Crystal Palace.
Rooney alipasuka Kichwani baada ya kugongana na Phil Jones Mazoezini na kumfanya aikose Mechi ya Man United na Liverpool hapo Septemba Mosi na pia Mechi za England dhidi ya Moldova na Ukraine.
Moyes amesema: “Yupo fiti. Jeraha lake limepona na Nyuzi zimetolewa lakini lazima tufanye tathmini ikiwa atacheza.”

Chanzo: http://www.sokainbongo.com
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.