.awaasa
vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao
.ashangaa
wajuzi walivyompachika jina la Ruksa enzi za miaka 1990s
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema kuna baadhi ya watu
katika jamii kutumia elimu, ujuzi na maarifa yao kuangamiza, kubomoa na
kudumaza ustawi wa jamii kwa maslahi binafsi na si ya umma. Mo blog inaripoti.
Mzee
mwinyi amesema hayo leo asubuhi wakati wa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya
amani duniani inayoadhimishwa 21th Septemba kila mwaka katika ukumbi wa Don
Bosco jijini Dar es Salaam, amesema kuna baadhi ya watu wanatumia elimu yao
vibaya kwa kupanga kuua watu wengine kwa maslahi yao aidha ya kisiasa au ya
kiuchumi.
“Elimu
kwa kawaida kuleta matokeo mazuri kwa jamii husika endapo itatumika sawia kwa
malengo yaliyokusudiwa na kwa maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla, ila kuna
baadhi ya wanajamii kutumia ujuzi huu vibaya na kuangamiza ustawi wa jamii husika,”
amesema.
Mzee
Mwinyi aliendelea kusema kwamba katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani
duniani yenye kauli mbiu “education for peace” ni lazima elimu kwa ajili ya
amani iwe endelevu hapa duniani ili iweze kuleta suluhu na utengamano katika
jamii na mataifa yote duniani.
Amesema
kwamba vijana nchini lazima waepuke kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao ya
kisiasa na wajifunze kutatua matatizo yao kwa njia ya amani bila ya kuwa na
mihemko, jazba, misongo na hasira ili kuendelea kudumisha amani na upendo
katika nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani.
“nawaasa
vijana wakitanzania wa leo hata kama mmenyimwa haki zenu ni bora kutumia njia
ya kistaarabu na kutumia elimu mnayopata mashuleni bila kusahau macho, masikio
na vipawa vyenu mlivyopewa na mwenyezi mungu katika kutafuta haki yenu kwa njia
ya amani bila misukosuko,” aliongeza.
Mzee
Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwashangaa baadhi ya watu kwa kutumia ujuzi na
elimu yao kwa kumpachika jina la Ruksa bila yeye kujua wametumia muktha gani
kumpa jina hilo, lakini Mzee Mwinyi alitumia jukwaa hilo pia kuwapa ruksa
vijana kutumia elimu yao kuleta hali ya amani na utulivu ndani ya nchi.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
(UNICEF) Jama Gulaid amesema kwamba Umoja wa Mataifa uliweka maazimio siku ya
kimataifa ya amani duniani ili watu wanaogombana na kupigana kwa shida
mbalimbali kupata nafasi ya kuweka silaha zao chini katika siku hii adhimu.
Amesema
kupitia azimio hilo ambalo lilizinduliwa mwaka 1982 kwa mara kwanza linatambua
uwepo wa watu wanaoathirika na vita katika sehemu mbalimbali duniani na
waliokwishapoteza maisha kutokana na matatizo vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Naye
Mratibu na Mtathimini wa Mtandao wa watoto na vijana kutoka Imani Mbalimbali
(GNRC) Bi, Joyce Mdachi amesema swala la amani na utulivu linaanzia kwenye kaya
hadi ngazi ya taifa kwahiyo ni muhimu kwa jamii na vijana kuelewa amani
inaanzia nyumbani.
“jamii
iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi kubwa ya kuleta matokeo chanya
kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla lakini jamii iliyolelewa vibaya haiwezi
kubadilisha taifa kwa sababu ni zao la tunda baya,” alisema.
Mdachi
alisisitiza kwamba kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii ya leo swala hilo pia
lilianzia kwenye kaya ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa ambapo leo hii
taifa linashuhudia mambo ya kifisadi, rushwa na ubadhilifu wa mali za umma
kunakofanywa na viongozi waandamizi.
Mwisho
Post a Comment