Timu ya Aston Villa jana usiku ilifanikiwa kulikimbia janga la kushuka daraja mara baada ya kuifunga timu ya Sunderalnd kwa jumla ya mabao 6-1. Itakumbukwa ya kwamba timu ya Sunderland tokea kumfukuza kocha wake na kumuajiri kocha mpya mwenye   matata na vituko vingi tokea akiwa mchezaji hadi kocha, Paul Di Canio ilishajipatia ushindi mfufulizo katika michezo yote miwili iliyokuwa imecheza chini ya kocha huyo.

Alikuwa ni mchezaji toka Ubelgiji , Christian Benteke aliyeifungia Astona Villa mabao matatu, " Hatrick" na kuishusha timu ya Newcastle hadi nafasi ya tatu kutoka mkia kwa kufikisha jumla ya pinti 37 sawa na Newcastle ila ikiwa na tofauti kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Naye kocha Di Canio asiyekosa maneno alisema," Wakati mwingine unapokuwa na chagula cha kutosha unapumzika" akiwa na maana ya kwamba timu yake ilibweteaka na ushindi mfufulizo katika michezo yake miwili iliyopita.


THE CLOCK STRIKES FOUR ... Big Ben rises highest to seal the win





























Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.