Timu ya Manchester United ya mjini Manchester jana usiku ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Engalnda kwa msimu wa 2012/2013 ikiwa kama kombe lake la 20 tangia kuanzishwa kwa ligi ya nchi hiyo. Ushindi huo mwanana ulichagizwa na mabao matatu maarufu kama "Hatrick" yaliofungwa na mchezaji wa kidachi Robin Van Persie, itakumbukwa mchezaji huyu alitokea Arsenal ambapo aliichezea timu hiyo ya Emirates kwa takribani miaka minane na hakuwahi kufanikiwa kuchukua kikombe chochote na timu hivyo kombe hilo litakuwa ni la kwanza kuchukua katika maisha yake ya soka.
Mchezaji wa Machester United, Robin Van Persie akishangilia moja ya mabao yake aliyoyafunga jana yalioiwezesha Manchester United kutangaza ubingwa wake wa 20 kwa msimu wa 2012/2013
Wachezaji Rio Ferdinand na Rafael Da Silva wakishindwa kuzuia furaha zao
Wachezaji wa Man United wakianza kushereheka ubingwa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo, picha na www.thesun.co.uk
Post a Comment