Chanzo cha kutimuliwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa
nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job
Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu
Nchemba (CCM).
Dodoma. Spika wa Bunge, Anne
Makinda amesema leo atatoa mwongozo kuhusu tukio la Naibu Spika, Job
Ndugai kuwasimamisha wabunge sita wa Chadema.
Juzi, Ndugai aliwasimamisha wabunge hao Tundu
Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji
Peter Msigwa (Iringa Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiah Wenje
(Nyamagana) na Godbless Lema wa Arusha Mjini kutohudhuria Bunge kwa siku
tano kutokana na alichokiita kufanya vurugu ndani ya bunge.
Hatua hiyo ya Spika Makinda imekuja baada ya
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kumtaka
aeleze Ndugai alitumia kanuni gani kuwasimamisha wabunge hao.
Jana, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbowe alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya 68(7) inayosema; “Hali kadhalika, Mbunge anaweza kusimama wakati wowote ambapo hakuna mbunge mwingine anayasema na kuomba “Mwongozo wa Spika” kuhusu jambo ambalo limetokea bungeni mapema, ili Spika atoe ufafanuzi kama jambo hilo linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na majibu ya Spika yatatolewa papohapo au baadaye, kadri anavyoona inafaa.”

Mbowe alisema Kanuni ya 73(3) ndiyo inayompa
ruhusa Naibu Spika na Spika kuwasimamisha wabunge na aliisoma: “Endapo
Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na
hadi kufikia mwisho wa muda alipopewa amekataa au ameshindwa kutoa
uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha mbunge huyo asihudhurie
vikao vya Bunge visivyozidi vitano.
“Kwa mujibu wa yaliyotokea jana (juzi) ilitokea
sintofahamu katika matumizi ya kifungu hiki wakati tulitegemea Kifungu
cha 74(1) ndicho kingetumika kwani kama mbunge amedharau mamlaka ya
Spika jina lake linaweza kupelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge,” alisema Mbowe na kuongeza: “Mheshimiwa Spika nataka
mwongozo wako kujua Naibu Spika alitumia kanuni gani?”
Awali, Spika Makinda aliahidi kutoa mwongozo wake
baadaye jioni kabla ya kuahidi kufanya hivyo leo wakati akiahirisha
shughuli za Bunge jana.
Awali, baada ya mwongozo wa Mbowe, Spika Makinda
alimruhusu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuomba mwongozo wake na
aliposimama alisema: “Mwongozo wangu uko palepale katika kanuni ileile
iliyoombwa na kiongozi wa kambi ya upinzani.”
Kabla hajamaliza, Spika alimkatisha na kumweleza kuwa hawezi kutoa nafasi ya mwongozo wa kitu hichohicho.
Alimruhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji
Frederick Werema ambaye alisema: “Waandishi walioandika kanuni hizi
kwamba jambo lilitokea mapema hawakumaanisha jana.”
Kabla Jaji Werema hajamaliza, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisimama lakini Spika alimzuia na kuwakatisha wote akisema: “Waheshimiwa wabunge, hakuna kitu kinachowaharibia wananchi kama kilichotokea jana (juzi), jana (juzi) hakuna kitu kilichojadiliwa zaidi ya kuleta zahama.”

Nchemba tena
Alimruhusu Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba kuendelea kutoa mchango wake ambao ulikatishwa kutokana na vurugu za juzi na jana nusura tena tafrani izuke kati yake na Mnyika hasa baada ya Nchemba kueleza suala la mabaraza ya Katiba kuwa utaratibu ulipitishwa bungeni na wabunge wote.

Alisema kinachotaka kujengwa na wapinzani hakipo
kwa kuwa katika Jimbo la Karatu lililoko chini ya upinzani, wenyeviti wa
mabaraza ya Katiba walichaguliwa wa CCM.
chanzo: Gazeti la Mwananchi
chanzo: Gazeti la Mwananchi
Post a Comment