NBC, yakutana na wadau wa PPF katika mkutano wao Arusha, Habari katika picha.
|
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PPF, Dk. Aggrey Mlimka
akibadlishana mawazo na Mkuu wa Hazina wa NBC, Pius Tibazarwa (kushoto),
katika hafla hiyo. NBC imesema wadau na wanachama wa mfuko huo ni kati
ya wateja wao muhimu hivyo hivyo hafla hiyo imewezesha pia kuwa karibu
nao, kuwafahamisha huduma mbalimbali zitolewazo na NBC. |
|
Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano wa NBC, William Kallaghe (kulia)
akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (kaikati) wakati wa
hafla hiyo. NBC imesema inathamini mchango mkubwa unaotoka kwa wadau na
wanachama wa PPF kuchangia maendeleo ya benki hiyo. Katikati ni Mkuu wa
Hazina wa NBC , Pius Tibazarwa |
|
Add caption |
|
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF),
Dkt. Aggrey Mlimka (Katikati), akisalimiana na Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano
wa Benki ya NBC, William Kallaghe (Kushoto), katika hafla ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wajumbe waliokuwa wakishiriki Mkutano wa 23 wa
Mwaka wa wanachama na wadau wa PPF jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu
wa Hazina NBC, Pius Tibazarwa. |
Post a Comment