kampuni inayoongoza katika vifaa vya teknolojia za mawasiliano kwa kushirikiana na RICOH kampuni ya kimataifa ya teknolojia zimeungana kibiashara katika kusambaza vifaa na bidhaa mbalimbali za sayansi na teknolojia hapa nchini.Katika ushirikiano huo,
kampuni hizo mbili kubwa katika biashara ya tekonolojia duniani wataweza kusambaza vifaa na bidhaa mbalimbali za uchapaji wa kisasa kwa kutumia teknolojia ili kuleta ufanisi katika ofisi za binafsi,
umma na mashirika mbalimbali Afrika Masharikina Kati.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo asubuhi jijini
Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Kampuniya Boss, Andrew Thompson
amesema ushirikiano huu utawezesha wao kutoa huduma katika ubora wa hali ya juu katika biashara ya kusambaza vifaa vya teknolojia hapa nchini.
Alisema kuwa ushirikiano huu nimuendelezo mzuri kwenye sekta binafsi hasa kwenye sayansi ya teknolojia ambapo mashirika mbalimbali wataweza kufanya shughuli zao katika mazingira
bora zaidi na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kupitia teknolojia habari na mawasiliano.
“katika dunia ya leo ya biashara,
kupunguza gharama katika biashara ni muhimu hasa kwa kutumia teknolojia,
tunapambana kwa ajili ya ufanisi, huku mashirika yakijipanga katika shughuli zao kila siku ili kukuza mitaji na uchumi wa kampuni husika,’
“
sisi kwa pamoja tuna furaha kujiunga na kampuniya RICOH,
ambayo inatumiwa na mashirika mengi duniani,
na ushirikiano huu utasaidia mashirika ya kitanzania kukua kwa kasi katika Nyanja za sayansi na teknolojia kwakupunguza gharama na kuongezamapato,” alisema.
Kwa upande
wake, Meneja mwandamizi wamaendeleo ya Biashara, Tobias Johansson alisema“tumepata faraja kubwa na sisi ni watu wenye bahati kupata yakusaidia maendeleo ya sayansi na teknolojia hapa nchini.
“pia tunasambaza vifaa vingi vya komputa kama
vile scanners, projectors, servers, storage equipments, fax mails, paper
shredders, laminating machines, and many more,’ alisema.
Post a Comment