Januzaj, mwenye Miaka 18, aliifungia Man
United Bao zote 2 walipoifunga Sunderland Bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi
Kuu England waliyocheza mwisho na hiyo ilikuwa ni Mechi yake ya kwanza
tu kuanza kwa Mabingwa hao wa England.
Akiongea mara baada ya kusaini Mkataba huo, Januzaj alisema: “Ni furaha kubwa kusaini Manchester United!”
Meneja wa Man United, David Moyes,
ameeleza kuwa Januzaj, ambae alijiunga na Klabu hiyo Mwaka 2011 akitokea
Anderlecht ya Ubelgiji, ni ‘Kipaji cha ajabu!’
Adnan Januzaj-katokea wapi mpka kupewa mkataba mnono wa miaka mitano (5):
.Mzaliwa wa Ubeljiji mnamo Tarehe 5 Februari 1995 kwa wazazi wazaliwa wenye asili ya kutoka Albania na asili ya kosovo mnamo mwaka 1995.
.Alijiunga na Timu ya vijana ya Anderlecht mnamo mwaka 2005 na kudumu nayo kwa takribani miaka sita (6).
Mnamo mwaka 2011,Adnan alijiunga na na timu ya Manchester United.
Akiwa na timu yake mpaya ya vijana wa Manchester United, Januzaj alizidi aling’ara sana kiasi ambacho kocha mstaafu wa wakati huo Mzee Sir Alex Ferguson alitamka wazi ya kuwa "Adnani ni Mchezaji mzuri mno mwenye uwiano mzuri sana kisoka!".
Wakati Ligi hiyo ikiwa ukingoni na huku Manchester wakuwa taayri washajitangazia ubingwa mapema, Mzee Fergie aliamu kumpanga akiwa benchi katiak mchezio wao wa mwisho dhidi ya Westbromwich Albion (WBA) ambayo ilikuwa ndio mechi ya mwisho ya Sir Ferguson kama kocha mara baada ya kutangaza kung'atuka.
Januzaj aliuanza msimu huu mpya chini ya kocha David Moyes katika michezo yake ya kirafiki barani Asia kwenye mchezo dhidi mastaa wa Hong Kong kwenye ya mchezo wa kirafiki na baada ya hapo kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi (Charirty Shiedl Cup) dhidi wa mabingwa wa kombe la FA Wigan Athtletic ambapo Mancehster walifanikiwa kushinda mabao 2-0 huku Adnan akitokea benchi..
Msimu huu, amecheza Mechi za Ligi, dhidi ya Crystal Palace hapo Septemba 14 na Capital One Cup akitokea Benchi lakini Mechi na Sunderland hapo Jumamosi ndio ya kwanza kuanza.
-Januzaj yuko huru kuichezea Belgium, Albania, Turkey na hata England
Mkataba wa sasa wa Januzaj ulitakiwa
kumalizika mwishoni mwa Msimu huu kitu ambacho kingemfanya Kinda huyo
awe huru kuihama Man United kwa fidia ndogo tu Mwezi Januari kwa vile
yuko chini ya Miaka 24.
Mara baada ya kusaini Mkataba mpya
utakaomweka hadi 2018, Januzaj alieleza: “Ni kama ndoto! Tangu nitue
hapa nilijiona nipo kwenye Klabu sahihi kabisa!”
Ingawa aliwekwa Benchi kwenye Mechi ya
mwisho kabisa ya Sir Alex Ferguson Msimu uliopita, chini ya Meneja mpya
David Moyes, Januzaj ndio amepata nafasi kubwa ya kucheza ambapo
alitokea Benchi na kucheza Mechi ya kugombea Ngao ya Jamii dhidi ya
Wigan Mwezi Agosti ambayo Man United walishinda 2-0.
Moyes ametamka: “Ni Kipaji cha ajabu!
Ametulia na mwenye uwezo wa kutoka wapinzani na hilo ni jambo kubwa kwa
Kijana wa Umri wake!”
Hadi sasa Januzaj hajaamua kwenye Timu
ya Taifa atachezea Nchi gani kwani yupo huru kuzichezea Belgium,
alikozaliwa, pamoja na Albania, Asili ya Wazazi wake, au Turkey,
wanakotoka Babu zake.
Pia, Januzaj, kwa mujibu wa Kanuni za
FIFA, ataweza kuichezea England ifikapo 2018 ikiwa atabaki Mkazi wa Nchi
hiyo hadi atimize Miaka 23.
Post a Comment