Shirika la habari la BBC limegundua kuwa takriban watu 50 kutoka Uingereza wana uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Shabaab na makundi mengine yanayohusika na ugaidi duniani.
Wapiganaji wa kikundi cha Al Shabab |
Wengi walio kwenye orodha hiyo
walisafiri kwenda nchini Somalia kupigana kwa niaba ya kundi hilo na wengine
kujaribu kuifanya safari hiyo ingawa hawakufanikiwa.
Al Shabaab, ambao makao yao makuu
ni Somalia walikiri kuhusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jengo la
kifahari la Westgate mjini Nairobi.
Mawakili wa familia ya kiingereza
ya mmoja wa watu waliosajiliwa kupigania Al shabaab ingawa aliuwawa baadaye,
wanachunguza kifo chake.
Abdukadir Mohamed Abdukadir ambaye anadhaniwa ndiye muunganishaji mkuu wa wapinaji wa kikundi hicho mjini Somalia na wa wale wa al-Qaeda mjini Yemen |
Majina 47 yaliyokusanywa na BBC
yalitoka kutoka kwa watu mbali mbali ikiwemo stakabadhi za mahakamani.Takriban watu 32 kati ya walio
kwenye orodha hiyo , wanashukiwa kujiunga na al-Shabaab ili kupigana , wakati
majasusi wa Marekani M15 walipowanasa wengine wakijaribu kusafiri kwenda
Somalia.
Wengine saba walitajwa katika
mahakama za Uingereza kwa kujaribu kwenda Somalia ingawa njama yao ilijulikana
na kutibuliwa.
Hali ya washukiwa hao haijulikani
lakini wanne bila shaka wameuawa.
Ni pamoja na Tufail Ahmed kutoka
Mashariki mwa London. BBC imegundua kuwa polisi waliifahamaisha familia yake
kwua alifariki akiwa nchini Somalia mwezi Novemba mwaka jana.
Familia yake imelitaka shirika
lisilo la kiserikali la charity Reprieve kuchunguza madai kuwa majeshi ya nchi
za Magharibi yalihusika na mauaji hayo,.
Wizara ya ulinzi imekataa
kuzungumzia swala hilo.
Wengine walishtakiwa kwa kuchangisha
pesa kwa niaba ya al-Shabaab, au kufanya mipango ya kuwasafirisha
Wanne kati ya wanaume hao
wamefariki wakiwemo wanaume walioonekana kwenye kanda ya video iliyotolewa na
al-Shabaab wiki moja iliyopita.
Mwisho
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment