Na Mwandishi Wetu
Timu ya CHADEMA ikiongozwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe ametembelea
kanda ya Magharibi Mkoa wa Tabora na kumfikisha katika jimbo la Igalula, wilaya
ya Uyui.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotufikia, Mhe Kabwe amekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya,
Miswaki, Miyenza na Kigwa.
Kabwe amesema wamezungumza kuhusu
changamoto ya usafiri wa reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na
askari kwa kunyanganywa mifugo yao, zao la tumbaku, maji safi na salama na
suala la mchakato wa kuandika katiba mpya.
“Kimsingi shughuli za kiuchumi za
wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo, hata hivyo ukosefu wa miundombinu
unafanya wananchi wasipate thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao,” amesema.
Amesema alipofika Kijiji cha Loya
aliona eneo kubwa lina miti ya mihama ambapo wananchi wanatumia tu mihama
wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya yanaharibika tu yenyewe.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe amesema lazima matunda haya yawe na matumizi ya kiviwanda ili
kukuza Uchumi na kutoa ajira kwa vijana.
Mwisho.
Post a Comment