HOTELI ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam yatoa msaada wa mashuka, mataulo kwa kituo cha Kulelea Watoto yatima cha SOS Children Villages katika muendelezo wao wa kusaidia jamii na watoto waishio katika mazingira magumu.


Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar, Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton, Bw, Florenso Kirambata amesema wameamua kugawa msaada huo kwa sababu wao ni sehemu ya jamii.


“Tumeamua kugawa msaada huu kwa kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nao vituo vingi vya kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za kuhahikisha watoto yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya kila siku,” amesema.


Amesema baadhi ya msaada uliotolewa ambao ni jumla ya piece 984 yakiwemo Mashuka, Duvet Cover (mazulia), mataulo ya kuogea, mataulo ya kusafishia, mataulo ya kujifutia mkono, Mataulo ya kuogea, Napkins na Foronya.


Mkurugenzi huyo Bw, Kirambata amesema Hoteli ya Double Tree imekuwa ikitoa msaada wa aina hiyo kila baada ya miaka miwili na mwaka uliopita zali liliwaangukia Hospitali ya Taifa Muhimbili na safari wameona watoe msaada huo kwa kituo cha SOS Children’s Villages nchini.


Historia fupi ya Kazi ya Vijiji SOS Watoto katika Tanzania ilianza mwaka 1984. Kipindi hicho aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,  Alhaji Ali Hassan Mwinyi, alikaribisha ombi toka kwa taasisi ya Kijerumani ya Hermann Gmeiner la kujengwa kituo cha kulelea watoto.



Makubaliano ya serikali na mfadhili yalisainiwa tarehe 25 Februari 1987. Kijiji cha SOS Children kilijengwa kati ya 1988 na 1990 na familia ya kwanza walikuwa na uwezo wa kuhamia katika nyumba za familia kati kati ya 1991.



Kwa sababu ya uhuru wa kisiasa , SOS watoto Vijiji pia iliamua kufanya kazi bara na visiwani SOS Children Vijiji Zanzibar  na  SOS Vijiji ya Watoto Tanzania bara na walianza rasmi mwezi Aprili 1997. Kijiji kwanza SOS Watoto Tanzania Bara kilijengwa mjini Arusha, kaskazini mwa nchi.

Captions:Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw, Florenso Kirambata akikabidhi msaada huo kwa National  Administrator wa Kituo cha SOS Children’s Village Tanzania  Bw. Hamoud Rashid.



Mwisho. Asante
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.