Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye madarakani amewahi kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC.
Taarifa hii bila shaka
imetafsiriwa na wengi kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru Kenyatta
kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC mwezi ujao.
Duru zinasema kuwa hofu kuwa
huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama.
Waziri Amina amesema kuwa Rais
Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa yeye ni
rais hali imebadilika.
Kenyatta anatakiwa na mahakama ya
ICC kuhusiana na uhalifu dhidi ya binadamu katika ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu mwaka 2007/2008. Bi Abdalla amesema hayo kwenye
mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika
kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.
Wakati huohuo, Kenya imekanusha
madai kuwa inashinikiza mataifa mbalimbali ya Afrika kujiondoa katika mkataba
wa Roma uliobuni mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC.
Waziri wa mashauri ya kigeni
nchini humo Balozi Amina Mohamed kuwa Kenya imekuwa ikishirikiana na mahakama
hiyo na hata Naibu wa Rais William Ruto kwa sasa yuko mjini the Hague
kuhudhuria vikao vya mahakama hiyo.
Matamshi ya Bi Amina yanakuja siku
chache tu kabla ya mkutano wa Marais wa Afrika utakaofanyika Ethiopia jumamosi
hii.
Bi Amina amesema kuwa Kenya
haijashinikiza nchi yoyote kuondoka kwenye mkataba wa Roma na kuwa mkutano wa
AU umeitishwa na nchi tofauti wala sio Kenya.
Kadhalika Amina amesema kuwa
Kenya haina nia yoyote ya kutoendelea kushirikiana na mahakama ya ICC.
Wakati huohuo mwanasheria mkuu wa
Kenya Githu Muigai amepewa fursa ya kuielezea mahakama ya ICC kwa nini bunge la
Kenya lilipitisha hoja ya kuitaka Kenya kujiondoa kutoka katika mkataba wa
Roma.
Majaji wanaosikiliza kesi dhidi
ya naibu rais wa Kenya William Ruto, wamesema kuwa maelezo ya Muigai yatasaidia
mahakama kuchukua hatua zaidi za kuwalinda mashahidi ambao tayari wametoa
ushahidi wao.
Jaji mkuu anayeongoza jopo la
majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya Ruto, Chile Eboe-Osuji,ambaye alieleza kuwa
wanajadili swala hilo na kuwa maelezo ya Muigai kuhusu mkakati wa serikali
kutaka kuiondoa Kenya kutoka katika mahakama ya ICC utawasaidia kufanya uamuzi.
BBC
Picha ya Amina Mohammed, waziri
wa mambo ya nje.
Mwisho
Post a Comment