Na Damas Makangale, Moblog —

MBUNIFU wa mavazi Vida Mahimbo wa jijini Dar es Salaam Jumamosi ya wiki iliyopita amezindua ‘Collection’ yake ya ‘Face of Summer 2014’ yenye muonekano wa rangi za Kimataifa.

Event ilianza mchana majira ya saa Sita mchana ambapo wadau wa masuala ya urembo walipata nafasi ya kuangalia Collection mpya New Khanga T-shirts and Jeans yenye rangi za Kimataifa inayoitwa ‘Face of Summer 2014’ sambamba na kujipatia ushauri wa bure wa namna ya kupaka Make Up pamoja na utunzaji wa kucha kutoka kwa wataalam waliobeba kwenye fani ya urembo.


“Nimekuwa kwenye tasnia ya mitindo na mavazi kwa takribani miaka minne na leo nimezindua ubunifu mpya wa mavazi inaoendana na rangi za kimataifa hasa kwenye T-shirts na jeans,” amesema Mahimbo Mahimbo amesema kwamba yeye ana tengeneza nguo hasa za kike lakini ambazo zinaweza kuvaliwa karibu kila siku na watu wa rika mbalimbali wa kimataifa na watu wa kawaida.
 

Zipo Make Up za kila aina zinazoendana na ngozi ya mteja ambapo pia unaweza kupata kwa bei Jumla na reja reja. Pichani wageni mbalimbali wanaopenda urembo wakiangalia Make up wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye Duka la Atsoko Beauty and Cosmetic lililopo Mikocheni jijini Dar.
Amesema kwamba ameamua kumchangua (Sing Bird) Shaa kama balozi wake kwa sababu ni mtu anayeweza kuwakilisha vyema kwenye sanaa kutokana na mavazi, muonekano na uelewa wake mkubwa katika mambo ya mitindo hapa nchini. 


Mahimbo alisisitiza kwamba tukio hilo la Jumamosi iliyopita imetoa nafasi kwa wateja wake wa ndani na nje ya nchi kuweza kuona collection yake mpya ya 2014 hasa khanga na jeans.


Katika tukio hilo alishirikiana Atsoko wa duka la vipodozi kuandaa ‘Face of Summer 2014’ katika kuwapa watu waliotembelea nafasi ya kuona kazi zake mpya za sanaa ya ubunifu, amesema  

Shaa alichaguliwa kuwa balozi wa tukio hili na waandaaji kutokana na kuwa na sifa ambazo wao walizihitaji. Vida Mahimbo, Shaa, Rio Paul na Mary.

Kwa sasa wateja wa nchini wataweza kupata bidhaa ya T-shirts Khanga na Jeans katika duka la Atsoko Beauty and Cosmetics zilizotengenezwa na Vida Mahimbo


Muonekano wa Duka la Atsoko Beauty and Cosmetics lililopo Mikocheni jijini Dar palipofanyikia uzinduzi wa ‘Face of Summer 2014’ Collection mpya ya Mbunifu wa Mavazi Vida Mahimbo. 
(Picha na Zainul Mzige, MoBlog)

Wateja wakiangalia collection mpya ya nguo za mbunifu wa mavazi nchini,Vida Mahimbo. 


Add caption
 
 

Mmoja wa wateja akisoma brochures za bidhaa za Atsoko Beauty and Cosmetic.....She is so fine....!

BIdhaa mbalimbali za urembo
 

Flora Chacha akimpaka Make up mhudumu wa Peroni kuleta muonekano mzuri zaidi kwa wageni waalikwa.


 
 
Mbunifu wa Mavazi Vida Mahimbo (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa ‘Face of Summer 2014’ (Song Bird) Shaa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Atsoko Beauty and Cosmetic Marie Englesson (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Duka hilo.

 
 
Mtaalam wa kucha Maryciana Naivasha (katikati) Balozi wa ‘Face of Summer 2014’ (Song Bird) Shaa pamoja na Mtaalamu wa urembo Duka la Atsoko Beauty and Cosmetic Flora Chacha wakibadilishana mawazo (kulia)

 
 
 
 
 
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.