Katika juhudi za kuendeleza sekta
ya elimu hapa nchini, Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi, Airtel imetoa
vitabu vya kiada kwa shule ya sekondari ya Nyasaka iliyopo jijini Mwanza.
Kampuni hiyo ya simu imetoa vitabu
vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa shule hiyo iliyopo jijini
Mwanza ikiwa ni muendelezo wa mradi wa shule yetu unaoratibiwa na kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
vitabu hivyo Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya ziwa, Bw. Raphaeli Daudi amesema
Airtel inathamini sana umuhimu wa elimu kwenye jamii na ndio maana ilizindua
mradi wa shule yetu kwa ajili ya kuzisaidia shule mbalimbali zenye uhitaji wa
vitabu.
"Sisi kama kampuni tunaelewa
fika jinsi elimu ilivyo na umuhimu mkubwa kwenye jamii, pia tunatambua ni jinsi
gani sekta ya elimu inaweza kuleta mapinduzi ya kifikra na ya kiuchumi kote nchini na ndio maana tunatoa vitabu hivi
kwa ajili ya kuendeleza elimu kote nchini" amesema Raphaeli.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa
shule ya sekondari Nyasaka, Bw. Yoweri Camilo amesema Airtel ni moja kati ya
makampuni yanayothamini elimu kwa ajili ya maendeleo ya jamii na ni kitu
ambacho kinapaswa kuigwa kwa makampuni mengine kote nchini.
"Kuchangia sekta ya elimu ni
kuiendeleza jamii nzima na Airtel imeweza kutambua umuhimu wa sekta hii na kuiendeleza,
Na huo ni mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine," alisema Camilo.
Hivi karibuni Airtel ilichangia
vitabu mbalimbali za sekondari ikiwemo Kazuramimba ya Kigoma, Kalangalala ya
Geita, Kasoma ya Musoma na Buyago ya Bukoba.
Kupitia mradi wa Airtel shule yetu,
Airtel mwaka huu imejipanga kutumia zaidi ya milioni 150/- kwaajili ya kusaidia
shule za sekondari nchini.
Mwisho
Post a Comment