Shirikisho la soka duniani FIFA limewajumuisha wachezaji 6 wa klabu ya Bayern Munich kwenye orodha ya wachezaji wengine 23 watakaowania tuzo la mchezaji bora zaidi mwaka huu.
Rais wa Shirikisho la soka duniani, Sepp Blatter


Jose Mourinho alijumuishwa kwenye kitengo cha mkufunzi bora zaidi mwaka huu licha ya kukosa kuiwezesha klabu ya Real Madrid kushinda taji lolote kubwa msimu uliopita, matokeo ambayo mkufunzi huyo ameyataja kuwa mabovu.


Mchezaji wa kipekee kutoka Uingereza ambaye aliteuliwa ni mchezaji wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale.


Mshindi wa tuzo la mkufunzi bora Afrika Stephen Keshi wa Nigeria hakufanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo huku mwafrika pekee kuteuliwa kuwania taji hilo akiwa Yaya Toure mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City.


Hamna waakilishi kutoka Asia ama CONCACAF

Wachezaji wa kimataifa kutoka Ujerumani Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger , Thomas Mueller na Phillip Lahm pamoja na mfaransa Franck Ribery na mchezaji wa Uholanzi Arjen Robben ndio wachezaji wa Bayern walioteuliwa.


Wengine waliojumuishwa kwenye orodha hiyo ni wachezaji maarufu kama Lionel Messi, Andres Ineasta na Cristiano Ronaldo.


Aliyekuwa mkufunzi wa Bayern Jupp Heynckes ambaye nafasi yake imechukuliwa na Pep Guardiola ameteuliwa kwenye kitengo cha wakufunzi bora zaidi baada ya kuongoza klabu yake kushinda ligi ya ujerumani ya Bundesliga, kombe la ujerumani na ligi ya mabingwa barani Ulaya.


Chanzo: BBC Swahili
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.