Ni kazi ngumu sana kuishi katika maisha ya uhuru wa kuwa na silaha halisi na silaha handia katika mazingira ambayo vitendo vya uhalifu vinaongezeka na askari polisi wanalaumiwa kwa kutokuwa makini katika kulinda usalama wa raia.

Jana, mtoto mmoja wa miaka 13, Andy Lopez Cruz, ameuawa Santa Rosa (kaskazini mwa California, Marekani) baada ya 

polisi kummiminia risasi kati ya 6 hadi 8 sekunde kumi tu baada ya kumwona mtoto ambaye waliripotiwa muda mchache kabla, kuwa mtoto huyo hajazoeleka kuonekana mtaani hapo na alikuwa amebeba silaha.

Picture Polisi walipousogelea mwili wa Andy ndipo walipong'amua kuwa alichokuwa amebeba ni mfano tu wa bunduki ya plastiki  (toy). Sekunde kumi na sita baadaye, polisi hao waliita huduma ya dharura kwa ajili ya msaada wa kimatibabu ili kuokoa uhai wa mtoto huyo lakini ilikuwa maji yemeshamwagika.

Andy alikuwa amevalia sweta lenye kofia iliyofunika kichwa (hood kama ilivyokuwa kwa Trayvon Martin) na alikuwa akielekea kwa rafiki yake kwa ajili ya kucheza na toys zao hizo.

Askari wa Kaunti ya Sonoma katika ofisi ya Sheriff waliohusika katika tukio hilo wamepewa likizo kupisha uchunguzi.

Haya yanatokea katika wakati ambapo kumekuwako mvutano mkubwa sana baina ya wale wanaounga mkono kudhibitiwa kwa aina ya silaha ambazo mtu binafsi anaruhusiwa kuwa nazo na wale wanaounga mkono haki ya Kikatiba ya kumiliki silaha ya aina yoyote kwa ajili ya kujilinda.

Mvutano unaendelea kutokana na matukio mbalimbali yaliyosababisha vifo vya watu wengi baada ya watu kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha binafsi katika ukumbi wa sinema, mashuleni na kwneye maeneo yenye shughuli za kijamii yenye mkusanyiko wa watu wengi.

Askari nao wamekuwa wakibebeshwa mzigo wa lawama kwa kushindwa kuifanya kazi yao kwa umakini ama kwa kutokuzuia uhalifu na madhara kwa binadamu au kwa ku-overreact na hivyo kujeruhi na kuua kwa kukosa umakini na kushindwa kuchukua tahadhari kwa matukio ambayo hayakuwa na hatari yoyote.

Source: http://www.wavuti.com

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.