Akizungumza na waandishi
wa habari jana asubuhi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja
Binafsi, Bw, Kumaran Pather alisema kuwa wanajivunia kuwa benki ya kwanza
nchini kutumia mfumo wa utoaji wa huduma za kibenki kwa mfumo huo mpya.
Alisema kwamba mfumo huo
wa kutoa huduma za benki bila kujaza fomu au karatasi ni moja tu ya huduma
mbalimbali ambazo benki hiyo inaleta katika kuboresha huduma zake kwa wateja.
“mfumo huu wa utoaji
huduma za kibenki bila kutumia karatasi unachukua nafasi ya matumizi ya
karatasi katika kupata huduma ikiwemo fomu mbalimbali za kutolea na kuchukulia
pesa,”
“uvumbuzi huu ni wa kisasa
na tunajivunia kwa sababu wateja wetu sasa hivi wanatumia chini ya dakika tatu
kuweza kukamilisha miamala yao ikiwemo kulipwa fedha taslimu, kuweka cheki,
kutoa pesa na kubadili hundi kuwa pesa taslimu,” alisema Bw, Pather
Bw, Pather aliongeza kuwa
uvumbuzi huu umesaidia kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa katika kuhudumia
wateja na pia inapunguza muda wa utoaji wa huduma kwa wateja.
Alisema kwamba mfumo wa
utoaji huduma bila kutumia karatasi inaweka hatua nzuri ya kuwezesha mteja
achanganuae cheki wa mashine ya elektroniki na baadaye utasaidia cheki
kukaguliwa na kifaa maalum, kupitiwa na kuidhinishwa na Benki kuu (Cheque
truncation).
Kwa upande wake, Meneja
Miradi wa Barclays Jane Mbwilo alisema benki hiyo inakuwa ya kwanza kutumia
mfumo huu nchini Tanzania na kuwa benki ya kwanza kutumia mfumo wa kupitisha
cheki kwa mitambo inayojiendesha yenyewe.
“Tumepiga hatua kubwa sana
katika kuboresha huduma kwa wateja wetu na mfumo huu mpya wa kutoa huduma bila
makaratasi, wateja wetu wote wanaweza kutumia mfumo huu katika matawi yote ya
Barcalys nchini,” alisema
Aliongeza kuwa mkakati wa
benki hiyo ni kutumia teknolojia ambayo itasaidia kurahisisha huduma kwa wateja
pia na kupunguza gharama za uendeshaji wa benki.
Post a Comment