WIKI Iliyopita Muungano wa asasi zisizo za kiserikali mbalimbali za kutetea haki za binadamu nchini kifupi AZAKI waliandaa mdahalo wa kwanza wa katiba jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na watu mashuhuri, vijana, wanafunzi wa kutoka vyuo vikuu mablimbali na kurushwa moja kwa moja na vituo kadhaa vya luninga hapa nchini, hongereni kwa kuwapa maarifa na uelewa watanzania wengi kuhusu mchakato unaoendelea wa kuandika katiba.
Kwa kutumia nafasi hiyo AZAKI ilitumia
fursa hiyo kuwafunda watanzania kwamba kila tunapofikiria au kuzungumzia kuhusu
katiba mpya, yanayojitokeza wazi kabisa ni Muundo wa Serikali, yaani mbili au
tatu.
Kwa mujibu wa AZAKI pia kwamba wenye
maslahi makubwa sana na katiba mpya ni CCM na UKAWA huku wananchi ambao
kimsingi ndio katiba yao wakiwa wameachwa solemba na wimbi la wanasiasa wenye
malengo yanayofanana hasa ni kutwaa madaraka na kupigiwa vingo’ra tu na kuu wa
kuhabutubiwa kwisheeeeeeee.
Kwa mujibu wa AZAKI wanasema kwamba
wananchi bado hawajawezeshwa kuifahamu Rasimu ya Pili ya Katiba, na kwamba
mchakato wa Katiba mpya umepoteza mwelekeo na hauna tena maslahi ya wananchi na
taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika mkutano wa AZAKI,
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu
alimtaka Rais Jakaya Kikwete kunusuru mchakato wa kupata katiba kwa kuwa yeye
binafsi ndiye aliyeuvuruga.
“Mchakato mzima ulikwenda vizuri, lakini
baada ya Kikwete kulihutubia Bunge Maalumu la Katiba, mwelekeo wa Bunge hilo
ulibadilika na kuwa na msimamo wa chama,” amesema Profesa Baregu.
Amesema kuwa Rais Kikwete alikwenda
kulihutubia Bunge kama kiongozi wa CCM, badala ya kiongozi wa nchi, ambapo
aliweka msimamo wa chama chake wa kutaka Muundo wa Serikali mbili na kuwavuruga
wajumbe ambao kimsingi ni wanachama wa CCM.
“Rais apate ujasiri akiwa kama kiongozi wa
nchi na siyo kama kiongozi wa CCM, awahutubie wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba na kuwataka wajadili Katiba ya wananchi na siyo ya chama wala yake
binafsi,” aliongeza Baregu.
Baregu aliwataka wajumbe watumie miezi
miwili iliyobaki kujipanga upya iwapo wana nia ya dhati ya kuendelea na
mchakato huo, ili ipatikane Katiba bora ya wananchi akionya kwamba, tofauti na
hapo Watanzania hawatakubali kuendelea kuburuzwa na misingi ya chama cha
mapinduzi.
Kauli ya Baregu pia iliungwa mkono na
Mwenyekiti wa Chama cha Sheria Zanzibar, Awadhi Ally Saidi ambaye ni pia ni
miongoni mwa waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, aliyesema kuwa
inafaa Rais awahutubie wajumbe na kuwakumbusha kuwa jukumu lao ni kujadili
Rasimu ya Katiba ya kuipitisha na siyo kuondoa vipengele au kubadilisha rasimu
au kufanya mambo kinyume na maoni ya wananchi.
“Ndiyo maana walipewa siku 70 kujadili
Rasimu ya Katiba, lakini walitumia siku 21 kutunga kanuni ambazo zilitungwa na
Baraza la Wawakilishi likishirikiana na Bunge la Muungano,” amesema.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa
kutetea haki za binadamu, Onesmo Olengurumwa ambaye pia ni mwanasheria amesema
kwamba makosa yalifanyika awali kwa kumuachia rais ateue wajumbe wa bunge la
katiba.
“kwa kufanya makosa ya kumwachia rais
ateue wajumbe wa bunge la katiba sasa bunge hilo limechepuka kutoka katika
nafasi yake na kutaka kubadili maoni ya wananchi na kuweka maoni ya chama
tawala,” amesema Olengurumwa
Amesema kwamba kwa sasa rais wan chi hana
nafasi ya kurekebisha makosa maana ameshakosea wenye jukumu hilo kwa sasa ni
wananchi wenyewe wa Tanzania kulirudisha bunge hilo kwenye mstari unaofaa.
Rais Jakaya Kikwete ameshauriwa kunusuru
mchakato wa kupata Katiba Mpya ili usisimame kwa kuvua koti la Uenyekiti wa CCM
na kubaki na Urais ili awaeleze wananchi nini cha kufanya kupata Katiba Mpya.
Ushauri huo umetolewa na viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa na wasomi walioshiriki katika mdahalo wa Katiba
uliofanyika jijini Dar es Salaam na Mwanza jana. Walisema kuwa Rais ana wajibu
kuunusuru mchakato huo kwa kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga kwa hotuba yake ya
ufunguzi wa Bunge Maalumu la Katiba iliyoonekana kuelemea upande wa chama chake
CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete amekuwa
kigeugeu juu ya Muundo wa Serikali za Muungano kama zilizopendekezwa kwenye
Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba.
Alisema kuwa Rais Kikwete alionyesha wazi
kukubaliana na Muundo wa Serikali tatu, kwani kabla Rasimu ya Pili ya Katiba
haijapelekwa kwenye Bunge Malaumu la Katiba ili kujadiliwa, alisaini kuonyesha
kuwa amekubaliana na yaliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Akihutubia kwenye Kongamano la Wazi na
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine
cha Mwanza (Saut) Dk Slaa alisema:
“Rais Jakaya Kikwete amekuwa kigeugeu,
kwani yeye ndiye aliyesaini Rasimu ya Pli ya Katiba ili ikajadiliwe kwenye
Bunge Maalumu la Katiba.” Aliongeza: “Kwa kuwa ndiye mtu wa mwisho kuruhusu
rasimu hiyo ijadiliwe kwenye Bunge Malaamu la Katiba ni wazi alikubaliana na
kilichopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyopendekeza Muundo wa
Serikali Tatu, hivyo inashangaza kuona leo anageuka na kutaka Serikali mbili.”
Dk Slaa ambaye pia ni kiongozi katika
Umoja wa Katiba ya Wananchi Nje ya Bunge (Ukawa), alisema kuwa katika mikoa 17
waliyozunguka na kufanya mikutano na wananchi, wamebaini kuwa Rasimu ya Katiba
ya Pili wananchi hawaifahamu na kwamba hiyo ni njia ya CCM kuchakachua maoni
yao yaliyomo kwenye rasimu hiyo, wakati wa kupiga kura za maoni.
Alisema wanatambua ujanja unaofanywa na
CCM kutaka kupitisha mambo wanayoyataka wao, lakini wao watendelea kuwaelimisha
wananchi ili watambue kwamba maoni yao ndiyo nguzo ya kuwapa Katiba bora na
siyo vinginevyo.
“Tumefanya mikutoano mikoa 17, lakini kote
tulipopita wananchi wametuambia hawaifahamu Rasimu ya Pili ya Katiba kutokana
na janja ya CCM kuficha rasimu ya hiyo ili wananchi wasiifahamu. Kutokana na
hilo ni wazi kwamba wanataka kuchakachua
maoni ya wananchi kwenye kura za maoni,”alisema Dk Slaa.
Akinukuu maneno kutoka katika hotuba ya
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 Dk Slaa alisema:
“Watu wapumbavu ni wale wanaoamini kwamba Katiba haibadiliki.”
Alisema lazima Katiba ibadilike na kwamba
wananchi ndiyo wenye Katiba, hivyo siyo busara kutaka kuchakachua maoni yao na
kuweka maoni ya chama au mtu binafsi.
Post a Comment