![]() |
| George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah Mwanajamii, Mwanasiasa, na mchezaji wa zamani aliyecheza kama mshambuliaji ,anatoka Liberia. |
Ilikuwa ni mwezi Desemba, mwaka 1995, ni pale FIFA ilipoitangazia dunia ya soka, kuwa George Weah amechaguliwa kwa kupigiwa kura kuwa mwanasoka bora wa dunia.

Na mwaka huo huo, George Weah akawa Mwanasoka Bora wa Ulaya, na haikuishia hapo, akatangazwa pia kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika! Mwaka mmoja mataji matatu!
George Weah alianza kusakata kabumbu nchini mwake Liberia kabla ya kuhamia klabu cha Monaco, na baadae Paris Saint Germain. Mwaka 1995 akaenda kwenye klabu ya Milan na ndipo akafikia kilele cha mafanikio yake katika soka. Kwenye uwanja wa nyumbani wa San Siro wa timu ya Milan, George Weah alikuwa mfalme aliyependwa sana na wapenzi wa Milan.
Pamoja na mafanikio makubwa katika soka, George Weah hakuwahi kushiriki
kucheza fainali za Kombe la Dunia. Na bila shaka, kwa kusukumwa na hamu
ya kuiona nchi yake ikiongozwa na mtu atakayeweza kuifanya itulie na
kuondokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na hata kucheza kombe la
dunia, mwaka 2005, George Weah akaamua ' kucheza kandanda ya majukwaa ya
siasa'. Alishiriki uchaguzi mkuu wa Liberia. Aligombea Urais wa
Liberia, Huko akakutana na wenye kujua ' kucheza siasa'.George Weah akagalagazwa na mwanamama Ellen Johnson - Sirleaf.

Post a Comment