Hayo yalisemwa na Kamishna wa Utawala na Utumishi wa Jeshi la Polisi
nchini, Thobias Andengenye katika wakati akipokea kwa niaba ya mkuu wa
jeshi hilo (IGP), msaaada wa tani 50 za saruji zenye thamani ya zaidi ya
sh milioni 12 kutoka Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha polisi cha Mbweni Malindi nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kamishna Andengenye alisema kuwa
hata kama wananchi wakijenga nyumba imara lakini kuna umuhimu wa kuwepo
kwa vituo vya polisi katika makazi ili kuweza kutoa msaada wa haraka
pindi uhalifu utakapotokea.
"Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la
Polisi, Ernest Mangu ambaye alipenda kuwepo mahali hapa nachukua nafasi
hii kuipongeza kampuni ya Twiga Cement kwa msaada huu, makampuni na
taasisi nyingine na bila kusahau juhudi za wananchi wa Kawe katika
kuhakikisha kituo hiki kinakamilika haraka," alisema.
Akizungumza
wakati akikabidhi saruji hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPCC, Alfonso
Rodriguez alisema msaada huo umewezeshwa kutoka na sera nzuri ndani ya
kampuni ya kuisaidia jamii inayowazunguuka na pia wanayofanya nayo
biashara.
"kama ilivyo kauli mbiu ya Twiga Cement isemayo
'Usalama Kwanza' ni matumaini yetu jamii ikiwa salama itakuwa rahisi
kuleta maendeleo yao kiuchumi na pia kufanya kuwezesha biashara yetu
iendelee vizuri," alisema.
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam , Suleiman Kova aliwapongeza wakazi wa
Mbweni kwa kutekeleza kwa vitendo dhana nzima ya ulinzi shirikishi.
Awali
alizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo
hicho, Reeves Ntalemwa alisema uamuzi wa kujitolea kujenga kituo hicho
kitakachogharimu sh milioni 700 hadi kukamilika ulioanzishwa na wananchi
wenye umetokana na kuongezeka kwa matukio ya uhalifu katika eneo hilo
linalopakana na Bahari ya Hindi.
Ukiacha kampuni ya Twiga, wadau
wengine wa maendeleo waliotoa misaada mbalimbali kufanikisha ujenzi huo
ni benki za CRDB PLC, NMB na NBC, wengine ni kampuni za VGK Ltd, Giant
Hill, IPTL, HISAJE na Ulotu.
Post a Comment