Hili linajadliwa kwa undani katika
sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with
Atitude.
Sinema hii ambayo inaoneshwa katika
ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya
kuhamasisha Watanzania kutambua kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa
migogoro inayowakuta na kwa kupitia elimu.
Women with Altitude inazunguka
katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini.
Baada ya kufanikiwa kupanda
mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal waliamua kupanda milima
mingine nmirefu katika mabara mbalimbali wakiwa na lengo la kutoa ushawishi kwa
wanawake na wasichana duniani kote kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni
magumu na hayawezekani.
Mtanzania mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya "Woman with Altitude" iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog). |
Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na documentary iliyopewa jina la “Women with Altitude” ambapo ndani yake wameshirikishwa wasichana wa kitanzania wawili na imefadhiliwa na shirika hilo itakayooyeshwa leo jioni ndani ya viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF 2014. |
Baadhi ya wasanii na waigizaji filamu wanaohudhuria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. |
Post a Comment