Redio za jamii nchini zimeaswa kutumika vizuri katika kuelimisha kamii
juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia vipindi vya redio.
|
Meneja wa kituo cha
Sengerema FM Redio, Ndg. Felician Ncheye, akitoa nasaha za ukaribisho
kwa washiriki wa mradi wa SHUGA na mgeni rasmi. Katikati ni Mgeni
rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia
mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu na Kulia ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI
UNESCO, Ndg. Herman Mathias.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog) |
Hamasa hiyo imetolewa na Ndg Geofrey Mabu ambaye ni mratibu wa UKIMWI halmashauri
ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS wakati akifungua warsha ya
siku tatu ya mradi mpya ujulikanao kama SHUGA, unaotekelezwa na shirika la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana Shirika la Mfuko wa
Watoto (UNICEF) inayofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani
Mwanza.
|
Mgeni rasmi Mratibu wa
UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS,
Ndg. Geofrey Mabu akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya
kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao
kama SHUGA. |
Mabu amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo malengo yake
yakizingatiwa na kutekelezwa kama ilivyopangwa utasaidia kufikia malengo ya
serikali ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi Zero.
Amesema kuwa redio za jamii ni kiungo muhimu katika kuelimisha jamii na
kuwa kama zitatumika vizuri kusambaza elimu ya UKIMWI kupitia vipindi vyake
zitasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali kupitia TACAIDS.
Vile vile ameziomba redio zitakazoshiriki katika mradi huu, kutumia
vizuri fursa hii waliyoipata kuhakikisha wanafanikisha malengo ya mradi kwa
kiwango cha juu kwa kufanya hivyo pia watakuwa wamelinusuru taifa na janga hili
la UKIMWI.
Awali Mkufunzi wa Radio za jamii kutoka shirika la UNESCO Bi Rose Mwalimu
akitoa ufafanuzi wa malengo ya semina hiyo, amesema kuwa mradi huu wa SHUGA
unalenga kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa vijana hapa
nchini kupitia vipindi vya mchezo wa redio kubadili tabia.
Amezitaja redio 10 zinazoshiriki katika mradi huu nchini Tanzania kuwa ni
FADECO Redio ya Karagwe mkoani Kagera, ORS ya Manyara, Sengerema FM mkoani
Mwanza, Pangani FM ya mkoani Tanga na Kahama FM kutoka Shinyanga.
Nyingine ni Kitulo FM ya Makete Njombe, Kyela FM ya Mbeya, Nuru FM kutoka
Iringa, Pambazuko FM Ifakara na Kwanza Jamii Redio FM kutoka Njombe.
|
Mshauri na Mkufunzi wa
Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa maelezo kuhusu
madhumuni ya warsha inayohusisha mradi wa SHUGA |
|
Afisa Mipango VVU/UKIMWI
UNESCO, Ndg. Herman Mathias akitoa mada kuhusu VIjana, Balehe na
Mahusiano ya Ngono wakati warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha
Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA. |
|
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi. |
|
Mshiriki kutoka Kahama FM Redio, Makunga Peter akiuliza jambo kutoka kwa mkufunzi (hayuko pichani). |
|
Picha juu na Chini ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI
kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akitoa mada kuhusu kiwango cha
Maambukizi ya VVU kwa Vijana na hali ya Afya ya Uzazi Salama wakati wa
mafunzo hayo |
|
Mshiriki wa warsha ya siku
tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi
mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA kutoka Sengerema FM Redio, Peter
Marlesa akijenga hoja kuhusu viashiria hatarishi vya maambukizi ya VVU
kwa vijana |
|
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi wa SHUGA wakiwa katika vikundi kazi. |
|
Mgeni rasmi Ndg Geofrey
Mabu wa TACAIDS, wakufunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa
warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa
Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA. |
chanzo cha habari na
Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog
Post a Comment