MAHAKAMA
Kuu Kanda Ya Dar es Salaam, leo itaanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa
na wanachama wa tatu wa Timu ya Soka ya Simba, ambao wanakomba
mahakama hiyo itoe amri ya Muda ya Kuzuia kufanyika kwa uchaguzi
Mkuu wa Timu hiyo ambao umepangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.
Akizungumza
na Tanzania Daima Jana mchana, Wakili wa wanachama Hao, Revocatus
Kuuli alisema uongozi wa Mahakama umempatia Jaji Augustine Mwarija
kuisikiliza na inaanza kusikilizwa kusikilizwa Leo.
Endapo
Jaji Mwarija atasikiliza Kesi hii Na.291/2014 Kama ilivyopangwa,
itakuwa ni Mara yake ya pili kusikiliza Kesi ya aina hiyo. Mara ya
Kwanza ilikuwa ni Mei 8 Mwaka 2010 ambapo Jaji Mwarija akiwa na wa
Mahakama hiyo alitoa amri ya kubatirisha amri ya muda ya kuzuia
uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika Mei 9 mwaka 2010.
Amri
ya kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa simba iliyotenguliwa na jaji
huyo ilitolewa Mei 6 mwaka 2010 na aliyekuwa Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Amiceth Wambura ambapo Jaji Mwarija Alisema
Amefikia uamuzi wa kutengua amri hiyo baada ya kubaini kuwepo Kwa dosari
Katika amri ile ya Mahakama ya Kisutu.
Amri hiyo ilitolewa saa 1:10 jioni
na Jaji Agustine Mwarija baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili
zilizokuwa zinavutana katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na Michael
Wambura dhidi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba, wa wakati huo, Hassan
Dalali, kuruhusu uchaguzi huo kuingiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF).
Juni
23 mwaka huu, wananchama Hao watatu kupitia Wakili wao Kuuli walifungua
mahakamani hapo Maombi hayo madogo, Na.291/2014 Josephat Waryoba,
Said Lly Monero na Hassan Hassan, ambao wanamshitaki Rais wa Timu ya
Simba, Ismail Aden Rage na Bodi ya Udhamini ya Timu hiyo.
Kwa
mujibu wa hati hiyo inayonyesha walalamikaji wana jumla ya Madai matatu
ambayo dai la kwanza wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya kuwazuia
wadaiwa kuitisha uchaguzi Mkuu uliofangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.
Wakili
Kuuli analitaja ombi la pili ni wanaomba jumla ya wanachama 66
waunganishwe Kwenye Kesi hiyo ili nao wawe walalamikaji dhidi ya wadaiwa
kwasababu wadaiwa ambao Rage na Bodi ya Wadhamini wamevunja Katiba
ya Simba , taratibu za uchaguzi na na maadili ya uchaguzi , kadi za
uanachama za wanachama hao zimearibiwa.
Wakili
Kuuli alidai kuwa mdaiwa wa kwanza Kamati ya Utendaji ya Simba
walishindwa kuweka sawa Kamati ya Maadili ya simba Kama inavyotakiwa
na Katiba ya Timu hiyo na Kanuni za uchaguzi za TFF.
Alidai
Kwa vitendo hivyo wadaiwa hao wamevunja taratibu zote za uchaguzi
na kwamba Hakuna Chombo Cha klabu ya Simba ambacho kimepewa madaraka
ya kusimama a masuala ya rufaa ya Maadili ya wanachama wake na kwamba
rufaa zote zote zinazohusu Maadili zinasimamiwa na mdaiwa wa pili(Bodi
ya wadhamini ya simba), nakwasababu hiyo wanaiomba Mahakama hiyo
itafsiri Hilo.
" Japo Kuwa maelekezo toka TFF kwenda mdaiwa wa kwanza (rage) ya
Yaliyomtaka
Rage aweke sehemu ya Kamati ya Maadili , Rage alishindwa kutekeleza
maelekezo hayo KWA Madai Kuwa robo Tatu ya wajumbe wa Kamati ya
Utendaji wa Timu hiyo , wanatuhumiwa KWA makosa ya utovu wa Maadili .
"
Barua ya TTF kwenda KWA Rage ya Mei 29 Mwaka huu ,na barua ya
Mwenyekiti wa Simbaya Juni 17 Mwaka huu ambayo alikuwa akimjibu Rais wa
TFF, Jamal Malinzi ni ambazo tumeziambatanisha katika hati yetu ya
madai kama vielelezo ili mahakama itoe tafsiri ya sheria " alidai wakili
huyo.
Aidha
walalamikaji hao wanadai Kuwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba ipo kinyume
na Katiba ya Timu ya Simba Kwani Kamati hiyo Ina baadhi ya wanachama
ambao walioteuliwa Na Kamati ya Utendaji na waliondolewa na Rais wa
Timu hiyo Katika Kamati hiyo kinyume Cha Sheria .
Pia
wamedai Kuwa Kamati ya uchaguzi ya simba haina mamlaka ya Kamati ya
Maadili ya kuwandoa baadhi ya wagombea Katika mchakato wa uchaguzi
Mkuu Kwani Kamati ya uchaguzi wa kuwachuja wagombea pekee na suala la
utovu wa Maadili na nidhamu ya mgombea jukumu Hilo limekabidhiwa
Kwenye Kamati ya Maadili peke na siyo Kamati ya Uchaguzi .
"Kwa
Sababu hiyo tunaimba Mahala hii itamke Kuwa utaratibu wote wa kuendesha
uchaguzi ndani Timu ya Simba ni batiri kwasababu umekiuka Katiba ya
Simba" Alidai Wakili Kuuli.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Juni 25 Mwaka 2014.
Post a Comment