Na Happiness Katabazi
JAJI Shabani Lila wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, Aliyekuwa
amepangwa kusikiliza rufaa iliyokuwa imekatwa na Kiongozi wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu , Sheikh Ponda Issa Ponda, amejitoa kusikiliza rufaa
hiyo kwa maelezo Kuwa Dhamira yake inamfanya ajione hawezi kusikiliza
rufaa hiyo.
Jaji Lila alitoa uamuzi huo mwishoni mwa wiki ambapo alisema Dhamira
yake haimtumi kusikiliza rufaa hiyo namba 89/2013 iliyokatwa na Mwomba
rufaa (Ponda) dhidi ya jamhuri inayo omba Mahakama Kuu itengue hukumu ya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9 Mwaka 2013, ambayo ilimtia
hatiani kwa kosa Moja la kuingia kwa jinai Katika Kiwanja Cha Chang'ombe
Markaz ambapo ilimfunga Kifungo Cha Mwaka mmoja nje na kumtaka awe
mtunza Amani na raia mwema lakini Agosti Mwaka na alikamatwa na
kufunguliwa Kesi ya uchochezi kwa Madai ametenda makosa ya uchochezi
wakati Akiwa ndani ya Maandalizi ya hukumu hiyo.
"Kwa Dhamira yangu hainitumi kusikiliza rufaa ya Ponda, nimerudisha
jarada la rufaa hii kwa Jaji Mfawidhi ili aweze kumpanga jaji mwingine
wa kusikiliza .....na pia nimelikataa ombi la Wakili wa Ponda, Juma
Nassor lilokuwa Linaomba Mahakama hii impange Jaji mmoja atayesikiliza
rufaa hiyo ya Ponda na ombi lilonalooamba Mahakama hiyo itoe amri ya
Kuzuia Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Ponda
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro isimame hadi rufaa iliyokatwa
na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, itakaposikilizwa
kuamriwa.
Ponda aliwasilisha mahakamani hapo ombi la Kuomba Mahakama hiyo itoe
amri ya Kuzuia Kesi ya uchochezi inayomkabili Morogoro ,isiendelee
kusikilizwa hadi pale rufaa yake aliyoikata mapema Mwaka Jana ya Kapinga
hukumu iliyotolewa Na Mahakama ya Kisutu Mei 9 Mwaka Jana, ambayo
ilimtia hatiani Kwa kosa la kuingia Kwa jinai Katika Kiwanja Cha Markas
Chang' ombe, ambapo Mahakama hiyo ilimfunga Kifungo Cha nje Cha Mwaka
mmoja, lakini Agosti Mwaka Jana, alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Morogoro akikabiliwa na Kesi mpya ya uchochezi na kutenda kosa
wakati yupo chini ya uangalizi wa Kifungo Cha Mwaka mmoja nje.
Hata hivyo Wakili wa Ponda ,Nassor alimwambia waandishi wa Habari Kuwa
licha Jaji Lilla alikataa ombi lake la kuomba Maombi mawili ya mteja
wake yapangwe wa jaji mmoja lakini Jaji Mfawidhi ameyapanga Maombi hayo
mawili ya Ponda yaani rufaa iliyokatwa na Ponda na ombi la kuomba Kesi
ya Uchochezi inayomkabili mTeja wake mkoani Morogoro, yamepangwa
kusikilizwa kwa jaji Mmoja aitwaye Lawrnce Kaduri ombi la kuomba Kesi
ya uchochezi iliyofunguliwa Morogoro dhidi ya Ponda itaanza kusikilizwa
Agosti 4 mwaka huu na rufaa yake Ponda itakuja kutajwa tarehe hiyo hiyo.
Mapema Juni Mwaka huu, Wakili Mwandamizi wa serikali Bernad Kongora
aliwasilisha pingamizi la awali mahakamani Linaomba Mahakama hiyo
itupilie Mbali maombi hayo ya Ponda yanayo omba Mahakama itoe amri ya
usikilizwaji wa Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa Katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Morogoro ya simama hadi rufaa yake itakapoamriwa kwasababu
ombi Hilo linalengo ya kuaribu muda wa Mahakama na halina Msingi.
Chanzo: Gazeti La Tanzania Daima la Jumatatu, Juni 30 Mwaka 2014.
Post a Comment