Mabasi yaendayo kasi |
Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imependekeza kiasi cha Sh500 kwa barabara za ndani, Sh700 kwa barabara kuu, Sh 800 kwa wanaounganisha safari zao kutoka barabara za ndani kwenda barabara kuu na Sh 900 kutoka barabara za ndani kwenda barabara kuu na kwenda tena barabara za ndani.
Pia, wanafunzi watalipa nusu ya nauli ya mtu mzima kulingana na ruti wanayokwenda. Akijibu
maswali ya wadau mbalimbali walioshiriki kongamano la wadau wa mradi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DART, Asteria Mlambo alisema wamefanya utafiti na kubaini kuwa wananchi wanalipa zaidi ya Sh1000 ili kufika mwisho wa safari zao.
Aliongeza kuwa watu wako tayari kulipa zaidi ya Sh400 wanayolipa sasa ili mradi wapate huduma bora ya usafiri.
Naye Mtaalamu wa Mfumo wa Nauli kwa Njia za Miamala (AFCS), Jeroen Kok alibainisha aina ya mabasi yatakayotoa huduma katika barabara kuu ya BRT kuwa ni yenye urefu wa mita 18 na uwezo wa kubeba abiria 50 waliokaa na 110 waliosimama.
Kok alisema Mabasi yatakayotoa huduma katika barabara za ndani yatakuwa na urefu wa mita 12 na uwezo wa kubeba abiria 40 waliokaa na wengine 90 waliosimama.
Pia, mwendokasi wa mabasi makubwa utakuwa wa kilomita 24 kwa saa.
Chanzo via gazeti la MWANANCHI
Post a Comment