Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos Santana "Jaja" amewasili jana mchana jijini Dar es salaam akitokea jijini Sao Paul tayari kwa kuanza kazi ya kuitumikia klabu ya Young Africans Sports Club kwa msimu wa 2014/2015.
Mchezaji , Geilson Santos Santanamara alipokuwa anatua katika uwanja wa kimataifa wa JKIA jiji Dar es Salaam jana na kulakiwa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo

Jaja ambaye alikua akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni mchezaji wa pili kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey Coutinho kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio Maximo.

Usajili wa wachezaji hawa ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans kuhakikisha msimu ujao unakua na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika.

Jaja anaungana na makocha wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo Andrey Coutinho katikaa msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na wachezaji wengine wazawa wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.

Leo asubuhi Jaja anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano mbalimbali itayowakabili.

Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.