AJALI za barabarani limekuwa ni tatizo kubwa na sugu nchini na tumeendelea kushuhudia ajali nyingi zikitokea na kupoteza maisha ya watu na kuacha maelfu wakiwa majeruhi na wengine kuachwa vilema wa maisha.

Tatizo la ajali nyingi nchini ni kutokana na uzembe wa madereva kunakosababishwa na kutokutii sheria za usalama barabarani kwa kiwango ambacho hakivumiliki kwa mustakabali wa taifa letu.

Huko nyuma mtaalamu mmoja kutoka Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba ajali nyingi hapa nchini zinasababishwa na binadamu yaani (Human Errors) na ni chache zinatokana na tatizo la miundombinu.

Kwa hiyo sisi kwenye blog ya Makangale Satellite tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini, kikosi cha usalama barabarani kusimamia sheria, kanuni na taratibu kwenye usimamizi wa vyombo vya moto ili kupunguza ajali zinazoepukika na kunusuru maisha ya watu na mali.

Kwa sababu tunajua fika kwamba tatizo la rushwa nchini hasa katika sekta ya usafiri ni kichocheo kikubwa katika kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Pamoja na mambo mengine madereva wasiotii sheria za barabarani wanafanya hivyo kwa sababu wanajua watatoa rushwa kwa askari wa usalama barabarani lakini ni muhimu kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini kutazama upya sheria hizi ili ikiwezekana kutoa adhabu kali ikiwemo ya kifungo cha angalau mwaka mmoja kwa makosa ya uzembe barabarani achilia mbali faini.

Hivi majuzi tumeshuhudia ajali kati ya bari la abiria na lori na takribani watu kumi na saba kupoteza maisha yao na wengine kadhaa kupata majeraha makubwa.
Wenzetu wa Afrika ya kusini wamebuni mfumo ujulikanao kama “Road Buddy” uliobuniwa na mjasiriamali anayejulikana kama Werner Van Der Westhuizen kwa kutumia teknolojia ya Cloud Computing.

Utendaji kazi wa mfumo huu ulibuniwa na Bwana Werner almaarufu kama “Road Buddy” ni kwamba mara hawa watumiaji wakuu wa barabara wanapokuwa wanakaribia magari kuna viashiria vinavyotoa ujumbe kuelezea hali hiyo nah ii ni kutokana na teknlogia iliyotumika katika mifumo hii ya Cloud Computing.

Kulingana na hali ilivyo katika nchi ambapo watu wengi wanajiuliza nini kifanyike ili kuliepusha taifa na madhara makumbwa yanayosababishwa na ajali hizi ambapo wengine wanashauri jeshi la Polisi kuziangalia sheria zake za barabari ambazo zimepitwa na wakati kulingana na mahitaji ya sasa ilikuendana na hali halisi iliyopo lakini pia kuna haja pia ya kuboresha miundo mbinu mingine kama  uufungwaji wa Camera za barabari (CCTV) na hivyo kurekodi matukio yote ya barabari na kuwanasa wale wote wanaouvunhja sheria za barabari.

Kwa wenzetu hali hii ya kusema kuna tatizola maofisa wasio waamininfu katika kupokea Rushwa litakuwa limetattuliwa kwa kiasi kwa kuwa endapo camera hizi zitafungwa na mtumiaji wa barabara akawa amevunja rekodi ni kuwa voucher ya faini itapelekwa kwenye akaunti yake na kutakiwa kulipa faini na kadhalika.

Pia ni muda muafaka pia kuangalia na technologia nyingine kama za Bwana Werner ambapo ni uhakika hadi kufikia huku ni kutokana na madhara mmbalimbali yaliyokuwa yanasabishwa na watumiaji wa barabara na waendesha vyombo vya moto ambapo vilisababisha hadi watu kama kufikiria mbinu kama hizi ili kujaribu kupunguza ajali  hizi za barabarani.

Basi la Morobest lenye na namba za usajili T 258 AHV lilipopata ajali ya kugongana uso kwa uso na Lori
na kuua Watu 17 katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma, Basi lilikuwa likitoka Mpwapwa kwenda Dar es salaam.

Swali kubwa linaloacha vinywa pasipo kujibiwa ni hatua gani zichukuliwe ili kukomesha ajali hizi pamoja na jitahidi mbalimbali zinazofuatwa na vyombo vya usalama barabarani lakini hali hii inakuwa bado haikomeshe tatizo hilo
Lori lenye namba za usajili T 820 CKU na tela yenye namba za usajili T 390 CKT lililokuwa likiendeshwa na Dereva wake Gilbart Lemanya na Tingo wake Mikidadi Zubery Omary ambao wote walifariki papo hapo
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Morobest katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma

Ajali iliyotokea siku ya jumamosi katika milima ya Kitonga Barabara kuu kuelekea mikoa ya Iringa na Mbeya

































































































































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.