NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2013/2014


Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia wataalamu wa kada za afya kuwa bado kuna nafasi za kazi katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wataalamu wa kada zilizoorodheshwa hapa chini wanatakiwa kuwasilisha maombi yao ili waweze kupangiwa vituo vya kazi:

Madaktari Bingwa/ Madaktari Bingwa wa Meno, Madaktari/Madaktari wa Meno, Mdaktari Wasaidizi/Madaktari Wasaidizi wa Meno, Matabibu/Matabibu wa Meno, Matabibu Wasaidizi, Mteknolojia wa Meno, Wafamasia, Watenolojia wa Dawa, Wateknolojia Wasaidizi wa Dawa, Maafisa Wateknolojia wa Maabara za Afya, Wateknolojia wa Maabara za Afya, Wateknolojia Wasaidizi wa Maabara za Afya, Maafisa Wauguzi, Maafisa Wauguzi Wasaidizi, Wauguzi, Maafisa Fiziotherapia, Wafiziotherapia, wateknolojia wa Macho, Wateknolojia Mionzi, Afisa Afya Mazingira, Afisa Afya Mazingira Msaidizi, Mhandisi wa Vifaa Tiba na Mteknolojia wa Vifaa Tiba.

Barua ya maombi iambatanishwe na nakala ya cheti cha kidato cha nne, cheti cha taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji wa kada zenye Mabaraza ya Taaluma wawasilishe vyeti vya usajili au leseni.

Mwisho wa kuwasilisha maombi tarehe 30/6/2014
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.