.wamepokea shilingi 80 bilioni katika mpango wa makazi kwa watumishi wa umma
Na Damas Makangale, Makangale Satellite
Kwa watumishi wa umma uanzishwaji wa Watumishi Housing
Company (WHC) ambao ni mpango wa makazi kwa watumishi wa umma ni mkombozi wa
kweli kwa ustawi wa maisha ya mfanyakazi wa serikali, asante kwa serikali ya
awamu ya nne kwa kuanzisha taasisi hii muhimu kwa ujenzi wa taifa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Company (WHC), Dakta Fred Msemwa akiwa amepozi ofisini kwake baada ya mahojiano. |
WHC ni taasisi inayojihusisha na uendelezaji miliki na
usimamizi wa uwekezaji katika miliki. Kampuni hii ya umma imepewa jukumu la
kuwa mtekelezaji mkuu wa mpango wa taifa wa makazi kwa watumishi wa umma na ina
jukumu la kujenga nyumba 50,000 nchi nzima.
Akizungumza na Makangale Satellite mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji mkuu wa WHC, Dkt Fred Msemwa amesema kuwa
nyumba hizo zitauzwa kwa mkopo nafuu wa muda mrefu kwa watumishi wa umma.
“Baada ya Benki Kuu kulegeza masharti ya mikopo ya
nyumba kwa hiyo sasa mtumishi wa umma haihitaji fedha ya kutanguliza (deposit)
ambayo ni tofauti na masharti yaliyopo sasa katika uuzaji wa nyumba kwa mikopo
ambayo yanamtaka mnunuzi atoe asilimia 10 mpaka 20 kama fedha ya utangulizi,”
amesema Dkt Msemwa
Amesema kwamba WHC ni taasisi ya umma yenye jukumu la
uendeleza makazi yaliyo bora kwa watumishi wa umma nchini na ilianzishwa mwaka
2013 na jukumu kubwa ni kuboresha na kujenga makazi ya watumishi wa umma nchi
nzima.
Dkt Msemwa alisisitiza kwamba serikali iliamua kuja na
utaratibu huo wa makazi kwa watumishi wake baada ya kuona kwamba kwenye nguvu
ya soko la makazi watumishi wachache wanaweza kumudu nyumba zinazouzwa na
taasisi za fedha kwa sababu ya riba kuwa juu.
Amesema kwamba mkopo katika nyumba hizi ni kwa miaka
hadi 25 na riba ya nyumba hizi ni asilimia 10 hadi 13 ukilinganisha na hali
ilivyo kwenye soko la sasa la nyumba nchini Tanzania.
Dkt Msemwa amesema kwamba ujenzi rasmi wa nyumba hizi za
watumishi wa umma zitaanza kujengwa mwezi oktoba mwaka huu sehemu mbalimbali za
nchi kama vile Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Arusha, Shinyanga, Mwanza, Tabora,
Dodoma, Morogoro, Mbeya, Lindi na Mtwara.
Amesema kwamba inakadiriwa kwamba kuna wafanyakazi
650,000 wanaofanya kazi kwenye mashirika na sekta ya umma ambapo wafanyakazi
10,000 sawa sawa na asilimia 2 tu tu waliopata mikopo ya nyumba.
Aliongeza pia WHC wameweza kufika hapo walipo baada ya
kupata Baraka ya kuwa chini ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni Mfuko wa
PPF, National Social Security Fund (NSSF), Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa
Umma (PSPF), LAPF, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali (GEPF), Mfuko wa
Bima ya Afya (NHIF) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Amesema pia kwamba kampuni hiyo ina jukumu la kusimamia
vipande vya uwekezaji katika miliki (Real Estate Investment Trusts –REITs).
“kila mtumishi wa umma atanunua nyumba kwa kupitia mkopo
kwa kuangalia kiwango chake cha mshahara kama mtumishi wa umma,” alisisitiza
Dkt Msemwa alifafanua kwamba tofauti kati ya WHC ni
mabenki na kampuni zingine ni kwamba wengine wanafanya biashara kwa kuangalia
faida ila taasisi wana malengo ya kuhakikisha mtumishi wa serikali anapata
makazi bora ya kuishi kabla na baada ya kustaafu.
Amesema kwamba kuanzia katika mkoa wa Dar es Salaam
nyumba zitajengwa Mabwepande, Magomeni na Kigamboni baada ya kukamilisha
taratibu zote kwa kushirikiana na serikali za mitaa na wizara ya ardhi na
maendeleo ya makazi ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na hati miliki (title
deeds).
Dira ya WHC ni “Makazi Bora kwa Watumishi wa Umma” na
Dhima kuwezesha watumishi wa umma kumiliki nyumba kwa njia ya mikopo nafuu na
kufaidi matunda ya uwekezaji katika miliki kwa kutumia wafanyakazi wenye weledi
katika usimamizi wa uwekezaji na uendelezaji miliki.
Mwisho.
Post a Comment