- UTANGULIZI
Baraza la
Mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 100 kilichofanyika tarehe 15
Julai, 2014liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Mtihani wa
Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika tarehe 05 – 21 Mei 2014. Matokeo
haya yamechakatwa kwa kutumia viwango vya alama na madaraja ya ufaulu
kama ilivyooneshwa katika Jedwali la 1 na la 2.
Jedwali la 1: Viwango vya Ufaulu.
Alama
|
Uwigo wa Alama
|
A | 75 – 100 |
B+ | 60 – 74 |
B | 50 – 59 |
C | 40 – 49 |
D | 30 – 39 |
E | 20 – 29 |
F | 0 – 19 |
Mtahiniwa
atahesabiwa kuwa amefaulu somo endapo atakuwa amepata angalau gredi D
(alama 30) katika somo husika. Hivyo, kiwango cha juu cha ufaulu katika
somo ni Gredi A ambapo kiwango cha chini cha ufaulu (pass) katika somo
ni Gredi D. Ufaulu katika gredi A, B+, B na C utakuwa ni ‘Principal
Pass’.
Jedwali la 2: Madaraja ya Ufaulu.
DARAJA
|
POINTI/VIGEZO
|
I
|
3 – 7
|
II
|
8 – 9
|
III
|
10- 13
|
IV
| Awe na angalau D mbili au ‘principal pass’moja isiyopungua C. |
O
| Aliyepata ufaulu chini ya D mbili |
Uzito wa alama katika Gredi; A=1, B+= 2, B=3, C=4, D=5, E=6 na F=7.
- USAJILI NA MAHUDHURIO
- Watahiniwa wote
Jumla ya
watahiniwa 41,968 waliandikishwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2014
wakiwemo wasichana 12,674 (30.20%) na wavulana 29,294
(69.80%). Watahiniwa wa Shule walikuwa 35,650 ikilinganishwa na
watahiniwa 43,231 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka 2013.
Kati ya
watahiniwa 41,968 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei
2014, watahiniwa 40,695 sawa na asilimia 96.97 walifanya mtihani na
watahiniwa 1,273 sawa naasilimia 3.03 hawakufanya mtihani.
- Watahiniwa wa Shule
Kwa
Watahiniwa wa Shule, kati ya watahiniwa 35,650 waliosajiliwa,
watahiniwa 35,418 sawa na asilimia 99.35 walifanya mtihani ambapo
wasichana walikuwa ni 11,022 (99.63%) na wavulana ni 24,396
(99.22%). Watahiniwa 232 (0.65%) hawakufanya mtihani.
- Watahiniwa wa Kujitegemea
Kwa upande
wa Watahiniwa wa Kujitegemea, kati ya watahiniwa 6,318 waliosajiliwa,
watahiniwa 5,277 sawa na asilimia 83.52 walifanya mtihani na
watahiniwa 1,041 sawa na asilimia 16.48 hawakufanya mtihani.
- MATOKEO YA MTIHANI
- Watahiniwa Wote
Jumla ya
watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa waliofanya
Mtihani wa Kidato cha Sita 2014 wamefaulu. Wasichana waliofaulu
ni 12,080 sawa na asilimia 97.66wakati wavulana waliofaulu
ni 26,825 sawa na asilimia 95.25.
Mwaka 2013 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 44,366 sawa na asilimia 87.85.
- Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa
wa Shule waliofaulu ni 34,645 sawa na asilimia 98.26 ya waliofanya
mtihani. Wasichana waliofaulu ni 10,900 sawa na asilimia 99.20 na
wavulana ni 23,745 sawa na asilimia97.84.
Mwaka 2013 Watahiniwa 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo.
- Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya
Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 4,260 sawa na
asilimia 80.73.Mwaka 2013 Watahiniwa wa Kujitegemea 4,124 sawa na
asilimia 53.87 walifaulu mtihani huo.
- UBORA WA UFAULU
Ubora wa
ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha
kuwa jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 wamefaulu
katika madaraja I – IIIwakiwemo wasichana 9,954 sawa na
asilimia 90.59 na wavulana 20,271 sawa na asilimia83.53.
Jedwali lifuatalo linaonesha ufaulu kwa kila Daraja kwa Watahiniwa wa Shule na kwa Jinsi:
- Daraja la Ufaulu
Wavulana Wasichana Jumla Idadi Asilimia Idadi Asilimia Idadi Asilimia I 2,232 9.20 1,541 14.02 3,773 10.70 II 6,179 25.46 3,452 31.42 9,631 27.32 III 11,860 48.87 4,961 45.15 16,821 47.71 IV 3,474 14.31 946 8.61 4,420 12.54 0 524 2.16 88 0.80 612 1.74
- UFAULU WA MASOMO KWA WATAHINIWA WA SHULE
Na. MASOMOWALIOFAULU 2013 WALIOFAULU 2014 IDADI ASILIMIA IDADI ASILIMIA 111 GENERAL STUDIES 16,507 38.53 32,590 92.44 112 HISTORY 18,987 97.33 13,308 99.90 113 GEOGRAPHY 20,578 96.87 19,089 99.48 114 DIVINITY 2,674 90.61 2,280 96.65 115 ISLAMIC KNOWLEDGE 705 57.36 436 73.28 121 KISWAHILI 11,840 96.95 6,384 99.98 122 ENGLISH LANGUAGE 11,081 93.61 8,111 99.04 123 FRENCH 88 91.67 59 98.33 125 ARABIC 801 82.32 443 93.86 131 PHYSICS 5,788 46.34 9,311 78.41 132 CHEMISTRY 13,809 83.87 15,340 95.78 133 BIOLOGY 9,181 87.05 10,693 97.57 134 AGRICULTURE 537 98.35 350 99.72 136 COMPUTER SCIENCE 74 80.43 94 98.95 141 BASIC APPLIED MATHEMATICS 7,827 49.48 11,370 77.39 142 ADVANCED MATHEMATICS 6,895 69.32 8,537 89.40 151 ECONOMICS 8,173 93.53 7,589 99.57 152 COMMERCE 1,573 88.57 821 99.76 153 ACCOUNTANCY 1,660 93.42 819 99.27 155 FOOD AND HUMAN NUTRITION 107 98.17 121 100
- SHULE ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI
Mchanganuo wa upangaji wa Shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30.
6.1 Shule kumi (10) bora
Na JINA LA SHULE IDADI YA WATAHINIWA MKOA 1 IGOWOLE S S 30 IRINGA 2 FEZA BOYS’ S S 60 DAR ES SALAAM 3 KISIMIRI S S 52 ARUSHA 4 IWAWA S S 39 NJOMBE 5 KIBAHA S S 167 PWANI 6 MARIAN GIRLS S S 138 PWANI 7 NANGWA S S 97 MANYARA 8 UWATA S S 30 MBEYA 9 KIBONDO S S 62 KIGOMA 10 KAWAWA S S 47 IRINGA
6.2 Shule kumi (10) za Mwisho
Na JINA LA SHULE IDADI YA WATAHINIWA MKOA 1 BEN BELLA S S 105 UNGUJA 2 FIDEL CASTRO S S 69 PEMBA 3 TAMBAZA S S 322 DAR ES SALAAM 4 MUHEZA HIGH SCHOOL 117 TANGA 5 MAZIZINI S S 97 UNGUJA 6 MTWARA TECHNICAL S S 103 MTWARA 7 IYUNGA TECHNICAL S S 158 MBEYA 8 AL-FALAAH MUSLIM S S 37 UNGUJA 9 KALIUA S S 237 TABORA 10 OSWARD MANG’OMBE S S 122 MARA
- WATAHINIWA WALIOFANYA VIZURI ZAIDI
- Watahiniwa Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Sayansi Kitaifa
Na. JINA JINSISHULEMKOA MCHEPUO 1 ISAACK A SHAYO M ST.JOSEPH’S CATHEDRAL DAR ES SALAAM PCM 2 DORIS ATIENO NOAH F MARIAN GIRLS PWANI PCM 3 INNOCENT SABBAS YUSUFU M FEZA BOYS’ DAR ES SALAAM PCB 4 PLACID EZEKIEL PIUS M MOSHI KILIMANJARO PCM 5 BENNI B SHAYO M ILBORU ARUSHA PCM 6 ABUBAKAR JUMA M MZUMBE MOROGORO PCM 7 MWAMINIMUNGU CHRISTOPHER M TABORA BOYS TABORA PCM 8 CHIGULU JAPHALY M MZUMBE MOROGORO PCM 9 HUSSEIN PARPIA M AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY DAR ES SALAAM PCM 10 RAMADHANI ALLY MSANGI M FEZA BOYS’ DAR ES SALAAM PCM
- Wasichana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Sayansi Kitaifa:
Na. JINA SHULEMKOA MCHEPUO 1 DORIS ATIENO NOAH MARIAN GIRLS PWANI PCM 2 MONICA E MTEI MARIAN GIRLS PWANI PCB 3 WEMA KIBANGA MARIAN GIRLS PWANI PCB 4 DEBORAH A MLAWA MARIAN GIRLS PWANI PCM 5 DOREEN P KASHUSHURA MARIAN GIRLS PWANI PCM 6 HEAVENLIGHT M MUNISI ST.MARY GORETI KILIMANJARO PCM 7 FRIDA MBILINYI MSALATO DODOMA PCM 8 AISHA A MNJOVU FEZA GIRLS’ DAR ES SALAAM PCM 9 GLORY KWEKA MSALATO DODOMA PCM 10 MULHAT AHMED SAID FEZA GIRLS’ DAR ES SALAAM PCM
- Wavulana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Sayansi Kitaifa:
Na. JINA SHULEMKOA MCHEPUO 1 ISAACK A SHAYO ST.JOSEPH’S CATHEDRAL DAR ES SALAAM PCM 2 INNOCENT SABBAS YUSUFU FEZA BOYS’ DAR ES SALAAM PCB 3 PLACID EZEKIEL PIUS MOSHI KILIMANJARO PCM 4 BENNI B SHAYO ILBORU ARUSHA PCM 5 ABUBAKAR JUMA MZUMBE MOROGORO PCM 6 MWAMINIMUNGU CHRISTOPHER TABORA BOYS TABORA PCM 7 CHIGULU JAPHALY MZUMBE MOROGORO PCM 8 HUSSEIN PARPIA AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY DAR ES SALAAM PCM 9 RAMADHANI ALLY MSANGI FEZA BOYS’ DAR ES SALAAM PCM 10 LUSEKELO A KIHESYA MPWAPWA DODOMA PCM
- Watahiniwa Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Biashara Kitaifa
Na. JINA JINSI SHULEMKOA MCHEPUO 1 JOVINA LEONIDAS F NGANZA MWANZA ECA 2 NESTORY MAKENDI M KIBAHA PWANI ECA 3 IMMA ANYANDWILE M UMBWE KILIMANJARO ECA 4 THERESIA CYPRIAN MARWA F LOYOLA DAR ES SALAAM ECA 5 GRACE DAVID CHELELE F LOYOLA DAR ES SALAAM ECA 6 BETRIDA J RUGILA F BAOBAB PWANI ECA 7 JACQUELINE V KALINGA F WERUWERU KILIMANJARO ECA 8 TAJIEL ELISHA KITOJO F ARUSHA ARUSHA ECA 9 SHRIYA SANJIV RAMAIYA F SHAABAN ROBERT DAR ES SALAAM ECA 10 MWANAID MWAZEMA F WERUWERU KILIMANJARO ECA
- Wasichana kumi (10) Bora kwa Masomo ya Biashara Kitaifa
Na. JINA SHULEMKOA MCHEPUO 1 JOVINA LEONIDAS NGANZA MWANZA ECA 2 THERESIA CYPRIAN MARWA LOYOLA DAR ES SALAAM ECA 3 GRACE DAVID CHELELE LOYOLA DAR ES SALAAM ECA 4 BETRIDA J RUGILA BAOBAB PWANI ECA 5 JACQUELINE V KALINGA WERUWERU KILIMANJARO ECA 6 TAJIEL ELISHA KITOJO ARUSHA ARUSHA ECA 7 SHRIYA SANJIV RAMAIYA SHAABAN ROBERT DAR ES SALAAM ECA 8 MWANAID MWAZEMA WERUWERU KILIMANJARO ECA 9 VAILETH KALAGO NGANZA MWANZA ECA 10 MARY ROBERT NGOWA NGANZA MWANZA ECA
- Wavulana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Biashara Kitaifa
Na. JINA SHULEMKOA MCHEPUO 1 NESTORY MAKENDI KIBAHA PWANI ECA 2 IMMA ANYANDWILE UMBWE KILIMANJARO ECA 3 KELVIN NZOWA KIBAHA PWANI ECA 4 KIBHULI MWITA KIBAHA PWANI ECA 5 PRINCE MBWATE MWAMBAJA ST.JOSEPH’S CATHEDRAL DAR ES SALAAM ECA 6 ERASTO SONELO KIBAHA PWANI ECA 7 JOEL MATHEW MHANA KIBAHA PWANI ECA 8 SADICK MWANGA LUHEYA KIBAHA PWANI ECA 9 SHEWISHI H RAYMOND UMBWE KILIMANJARO ECA 10 ANTONY VICENT MUSHI UMBWE KILIMANJARO ECA
- Watahiniwa Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Lugha na Sanaa Kitaifa
Na. JINA JINSISHULEMKOA MCHEPUO 1 LISA VICTOR MIMBI F ST.MARY GORETI KILIMANJARO EGM 2 ROSALYN A TANDAU F MARIAN GIRLS PWANI EGM 3 JOSEPH NGOBYA M ST.JOSEPH’S CATHEDRAL DAR ES SALAAM EGM 4 ANETH D MTENGA F MARIAN GIRLS PWANI EGM 5 IDDA MICHAEL LAWENJA F MARIAN GIRLS PWANI HGL 6 EDNA EMMANUEL MWANKENJA F KISIMIRI ARUSHA HKL 7 CATHERINE J KIIZA F ST.MARY’S MAZINDE JUU TANGA HKL 8 NANCY ADON SWAI F MWIKA KILIMANJARO EGM 9 MOHAMED SALMIN M MWANZA MWANZA HGK 10 IDRISA HAMISI M MWEMBETOGWA IRINGA HGL
- Wasichana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Lugha na Sanaa Kitaifa
Na. JINA SHULEMKOA MCHEPUO 1 LISA VICTOR MIMBI ST.MARY GORETI KILIMANJARO EGM 2 ROSALYN A TANDAU MARIAN GIRLS PWANI EGM 3 ANETH D MTENGA MARIAN GIRLS PWANI EGM 4 IDDA MICHAEL LAWENJA MARIAN GIRLS PWANI HGL 5 EDNA EMMANUEL MWANKENJA KISIMIRI ARUSHA HKL 6 CATHERINE J KIIZA ST.MARY’S MAZINDE JUU TANGA HKL 7 NANCY ADON SWAI MWIKA KILIMANJARO EGM 8 HADIJA YUSUPH NGONYANI MWANZA MWANZA HKL 9 VICTORIA R NDOSI ASHIRA KILIMANJARO HGE 10 ZUHURA SHABANI MKILALU MARIAN GIRLS PWANI EGM
- Wavulana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Lugha na Sanaa Kitaifa
Na. JINA SHULEMKOA MCHEPUO 1 JOSEPH NGOBYA ST.JOSEPH’S CATHEDRAL DAR ES SALAAM EGM 2 MOHAMED SALMIN MWANZA MWANZA HGK 3 IDRISA HAMISI MWEMBETOGWA IRINGA HGL 4 SELEMAN RAPHAEL NDIKIMINWE HUMURA KAGERA HKL 5 SUNDAY MWAKIPAGALA ALPHA DAR ES SALAAM EGM 6 ERASTO EMMANUEL KISIMIRI ARUSHA HKL 7 MASHAURI FURAHISHA FAUSTINE MWANZA MWANZA HKL 8 EBBY EBAYOTH MALILA UWATA MBEYA HKL 9 CHARLES M ALBERT PUGU DAR ES SALAAM EGM 10 JOSEPH BASILIO KAWAWA IRINGA HGK
- MATOKEO YA MTIHANI YALIYOZUILIWA
- Watahiniwa 150 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa.
- Watahiniwa 9 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa katika Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.
- Watahiniwa 29 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.
- MATOKEO YA MTIHANI YALIYOFUTWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya watahiniwa wawili (02) waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani.
Baraza la
Mitihani la Tanzania linapenda kutumia fursa hii kuzipongeza Kamati za
Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Wilaya, Wakuu wa Shule na Wasimamizi wa
Mtihani uliyofanyika Mei, 2014 kwa kuzingatia na kusimamia taratibu za
Uendeshaji Mitihani vizuri na hivyo kuzuia udanganyifu kufanyika. Aidha,
Baraza linawapongeza watahiniwa wote waliofanya Mtihani wa Kidato cha
Sita, 2014 kwa kutojihusisha na udanganyifu.
- Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika Mei 2014 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
- www.necta.go.tz au www.moe.go.tz na
- Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA_KITUOXNAMBA_MTAHINIWA
(Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt. Charles E. Msonde
Post a Comment