NAIROBI, KENYA, Wagombea watatu wa wadhifa wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa eneo la Mathare tayari wameidhinishwa na tume ya Uchaguzi IEBC, kuwania kiti hicho.

Miongoni mwa walioidhinishwa ni George Wanjohi  wa TNA ambaye anatazamia kukinyakua kiti hicho tena baada ya kukipoteza kupitia rufaa iliyowasilishwa mahakamani.

Wengine walioidhinishwa ni Steven Kariuki wa ODM na Barrack Obath ambaye ni mgombea huru.

Haya yanajiri wakati mgombea huru wa wadhifa huo Gor Semelang’o akiwa tayari amemwandikia mwenyekiti wa wa IEBC akilalamikia kukandamizwa na mahasimu wake ambao wanasambaza mabango yanayomhusisha na muungano wa Jubilee yakiwa na picha yake pamoja na ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Uchaguzi huo mdogo utakaoandaliwa tarehe 7 mwezi Agosti mwaka huu, umewavutia wagombea 11.

 


.





































Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.