April 6, 202507:03:45 PM

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewaomba wapiga kura wake kumuombea kila siku kutokana na madai kuwa amekuwa akiwindwa na watu wanaotishia uhai wake.

Mnyika alitoa kauli hiyo juzi jioni katika eneo la Mbezi mjini Dar es Salaam wakati akihutubia mkutano wa hadhara:
“Nimekuwa nikizungumza mambo mengi ninapokuwa bungeni Dodoma, hasa ninapowatetea wananchi na wapiga kura wangu, lakini kuna watu hawafurahishwi kabisa…sasa wamefikia hatua ya kunitishia maisha yangu.
“Wengi mnakumbuka kwamba, Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Steven Ulimboka, alitekwa na kupigwa na watu wasiojulikana na kisha kung’olewa meno, baada ya tukio lile aliyekuwa akifuatia nilikuwa mimi, sasa sijui na mimi wanataka kunifanyia hivyo au la,” 
alisema Mnyika na kuongeza kuwa taarifa za yeye kutishiwa maisha zilianza kuvuja baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge la Bajeti.

Imeandikwa na Na Veronica Romwald, imechapishwa gazetini MTANZANIA
Labels:

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

Post a Comment

    Author Name

    Contact Form

    Name

    Email *

    Message *

    Powered by Blogger.