Utangulizi:
Jumatatu
na Jumanne ya wiki hii, kumekuwa na taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya
gazeti la kila siku zikieleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando
Mchechu ameundiwa zengwe na Bodi ya Wakurugenzi ya NHC kwa nia ya kuhakikisha
kuwa harejeshwi tena katika wadhifa huo, hasa baada ya Bw. Mchechu kumaliza
muda wake wa kuliongoza Shirika hili.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe akisoma
taarifa ya shirika hilo kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja
la kila siku na mitandao ya kijamii kuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw.
Nehemia Mchechu Kyando ameundiwa zengwe na baadhi ya wabunge ili
aondolewe katika shirika hilo, wanaofuaia katika picha ni Muungano
Saguya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii, Bw. Martin Mdoe Mkuu
wa Kitengo cha Sheria na Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki |
Aidha,
gazeti hilo liliwaaminisha umma wa watanzania kuwa mizengwe hiyo inaungwa mkono
na vigogo wa Serikali wakiwemo Wabunge ambao kuwepo kwa Bw. Mchechu katika
Shirika kumewanyima ulaji ikiwemo kupangishwa nyumba za Shirika. Gazeti
lililienda mbali zaidi likidai kuwa Bw. Mchechu amewekewa masharti magumu na
Bodi hiyo ya kumtaka apunguze idadi ya Wakurugenzi wa Menejimenti ya sasa ya
Shirika.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe akisoma taarifa ya NHC kulia ni Mpnda Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi . |
Kwa kuwa habari hizo zimeleta mtafaruku katika
Shirika na zimesababisha umma kuwa na mijadala mbalimbali juu ya jambo hili,
tungependa kuwataarifu umma kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, na Shirika
la Nyumba la Taifa linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-
1. Kwanza, ifahamike kuwa Bodi ya Wakurugenzi
ya NHC ina miezi miwili tu tangu iteuliwe na Mamlaka husika na haijawahi kukaa
katika kikao chochote kujadili suala la kumuondoa Mkurugenzi Mkuu na kupunguza
Menejimenti ya Shirika iliyopo sasa.
2.
Tunapenda kuwafahamisha kuwa Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya Shirika bado
wana mikataba halali ambayo haijamalizika muda wake, hivyo hoja ya kuwa Bwana
Mchechu na Menejimenti yake wanaundiwa zengwe baada ya kumaliza muda wao haina
ukweli wowote.
3. Kwamba kutokuwepo kwa Mkurugenzi Mkuu
kwenye ufunguzi wa miradi hakukutokana na kuwepo mizengwe kama ilivyoripotiwa
na Gazeti hili. Bw. Mchechu alikuwa katika likizo yake ya mwaka iliyooanza
tarehe 30 Juni na kumalizika Julai 18, 2014.
Likizo
hii ni stahili halali ya Bw. Mchechu kama walivyo watumishi wengine wa umma, na
hakuichukua likizo hii kutokana na kuwepo mizengwe ya kumuondoa kama
ilivyoripotiwa na Gazeti hili. Kuanzia tarehe 21 Julai, 2014 Bw. Mchechu yupo
kikazi nje ya nchi na anatarajiwa kuwa ofisini kwake tarehe 28 Julai, 2014.
4. Mwisho, tunapenda kuwatanabaisha wanahabari
kuwa kama ilivyo kawaida yetu, NHC imekuwa na itaendelea kuwa mstari wa mbele
kutoa habari makini kwa vyombo/chombo chochote cha habari bila kuficha jambo
lolote.
Hivyo,
tunawaomba muendelee kuitumia vyema fursa hii kupata habari zenye ukweli na
zilizo sahihi kwa jambo lolote mnalohitaji kuufahamisha umma wa watanzania.
Kwa
kufanya hivyo, tutaendelea kuwa washirika wakubwa wa vyombo vya habari, tukizingatia
kuwa vyombo vya habari vina dhima na dhamana kubwa katika kuleta tija kubwa kwa
Shirika na Taifa letu.
Aidha,
tunawafahamisha wateja wetu kuwa hakuna mtafaruku wowote uliyopo ndani ya
Shirika la Nyumba la Taifa na kwamba tunaendelea kuwapa huduma zetu zilizo bora
katika sekta ya nyumba tuliyoaminiwa na Taifa kuisimamia.
IMETOLEWA NA: BW.
DAVID SHAMBWE, KAIMU MKURUGENZI MKUU,
Post a Comment