TAASISI ya Hawzat-Imam-Swadiq (A.S), iliyopo Kigogo Post, jijini Dar es
Salaam, imepanga kufanya maandamano kesho kupinga mauaji yanayoendelea
Mashariki ya Kati dhidi ya Wapalestina.
Profesa Abdul Shariff (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo kuhusu maandamano ya amani ya kupinga ukandamizaji wa vikosi vya Israel dhidi ya Wapalestina vinavyoendelea jijini Gaza, Maandamano hayo yatakayofanyika kesho yataanzia Ilala Boma hadi Kigogo jirani na kituo kidogo cha polisi. Maandamano hayo ya kupinga mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya Palestina yameandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Hawzat-Imam Swadig (AS).Kulia ni Sheikh Hemedi Jalala. |
Mkuu wa taasisi hiyo, Hemed Jalala, akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, alisema wanapinga vikali mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya
Wapalestina na kuamua kufanya maandamano yataanzia katika kituo cha
daladala cha Ilala Boma hadi Kigogo uwanja wa Bibo kuanzia saa tatu
asubuhi hadi sita mchana.
“Hadi sasa maelfu ya Wapalestina wamepoteza maisha, hivyo jamii na taifa kwa ujumla tunapaswa kushirikana na kuonyesha kuguswa na mauaji hayo, kwani waathirika ni
watu wa dini zote.
“Kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo, watu wanashindwa kwenda misikitini na makanisani kufanya ibada na hata kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.”
Jalala alisema maandamano hayo yatahusisha watu wa dini zote na yana
kibali kutoka Jeshi la Polisi na kuiomba jamii kujitokeza na
kushirikiana kuonesha hali ya umoja kupinga mauaji hayo kwa kuwa
kunyamazia tatizo hilo ni kufanya kosa kwani hakuna hata dini moja
inaruhusu mauaji ya binadamu mwingine.
Msemaji wa Taasisi hiyo Profesa Abdul Shariff, amesema kuwa wameamua
kupaza sauti zao kulaani baada ya kuona Jumuiya mbalimbali za Kimataifa
ikiwa imenyamaza huku mamia ya watu wakizidi kupoteza maisha.
Amesema
kuwa inasikitisha kuona hata vyombo vya habari hasa vya Magharibi
havitoi nafasi kubwa kwa mauaji hayo ukilinganisha na mauaji yaliyotokea
kwa kulipuliwa kwa ndege Malyasia.
Viongozi na Mabalozi wa nchi
mbalimbali wamealikwa ili nao waweze kushiriki katika kupaza sauti zao
pamoja na Watanzania kulaani vitendo vinavyofanywa na Israel vya kuua
watu wasio na hatia.
Chanzo cha habari na mtandao wa www.wavuti.com
Post a Comment