Tafiti zimebaini kwamba Vijana hawatumii Kondomu na hutoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kutopata ladha wakati wa tendo la ndoa na kwamba inapunguza nguvu na visingizio vingine vingi vinavyopelekea kuashiria hatari ya maambukizi.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa |
Hayo
yameelezwa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw.
Herman Mathias wakati akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana
wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na
Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya
kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa
vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio.
“Asilimia
40 ya Wasichana na Asilimia 47 ya Wavulana ndio wenye ufahamu wa kina juu ya
maambukizi ya VVU huku asilimia kubwa wakiwa hawana elimu ya kutosha na hawajui
afya zao kwa kuwa hawana utamaduni wa kupima VVU”, amesema Bw. Mathias.
Katika
warsha hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNICEF
katika kituo cha Redio cha Nuru FM Iringa, Bw. Mathias amesema kuna umuhimu
mkubwa wa kutoa elimu sahihi kwa Vijana ya kujikinga na maambukizi ya VVU na
Mimba kutokana na uelewa mdogo wa Vijana katika matumizi sahihi ya Kondomu.
Wakichangia
mada kuhusu masuala muhimu yanayowahusu vijana katika maambukizi ya VVU vijana
wamesikitishwa na mimba za utotoni kwa wasichana zinazochangia vifo vya Mama na
Watoto na wasichana kuacha masomo.
Washiriki
wa warsha hiyo wametaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha kuwa sheria za
mtoto zinazoruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo zinafanyiwa
marekebisho ya haraka kulinda haki ya mtoto wa kike.
Wakijadili
mada hiyo washiriki wamesema mila na tamaduni pia zinachangia kwa kiasi kikubwa
kumkandamiza mtoto wa kike katika masuala mbalimbali ya maendeleo yake.
Wakitoa
mifano ya baadhi ya mila zilizowafanya wapaze sauti kuhusu mabadiliko ya sheria
za mtoto ni ile sheria ya ndoa na mila inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa
na umri wa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi. Umri huo unakinzana na haki za mtoto
kufurahia maisha yake na kupata elimu.
Mifano
mingine ya kitamaduni ni pale mwanamume anapochumbia mimba wakati akijua wazi
mtoto ana haki zake za msingi za kuishi.
Wamezitaja
pia asasi za dini kutoa elimu kwa vijana ili kusaidia hali iliyojitokeza ya
wazazi kutokuwa na muda na watoto wao kuwaelimisha kuhusu mabadiliko ya miili
na afya zao.
Akitoa
mada kuhusu mbinu mbalimbali za kuwezesha majadiliano katika vikundi vya
wasikilizaji, Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdul Mfuruki amewataka
wawezeshaji kutotumia nafasi walizonazo ili kuendesha mjadala wenye tija.
Amesema
washauri wa vikundi hawana budi kuweka mizania kutumia busara, kusoma mazingira
na kutoingiza imani au itikadi itakayopelekea kuharibu mjadala unaoendeshwa wa
kufuatilia vipindi vya SHUGA Redio, kuwa wavumilivu, kusoma na kuheshimu mawazo
ya wengine na kutofungamana na upande wowote ili kumweleza mshiriki wa
majadiliano kufunguka zaidi.
Bw.
Mfuruki amesema vijana wa vikundi vya wasikilizaji kuwaza mambo mengi ni vyema
kuwasikiliza kwa uvumilivu, kupata ushauri wa wengi kwa lengo la kufanya
maamuzi sahihi bila kulazimishana na vile vile kuwa wabunifu kwa kutumia mbinu
mbadala ili kupata habari iliyojificha.
Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akiwapiga msasa washauri wa Vikundi vya Vijana kwenye warsha ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa. |
Mmoja wa washiriki akihoji jambo kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo. |
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akifafanua jambo kwa washiriki. |
Pichani juu na chini ni Washiriki wakijidiliana kwenye vikundi kazi wakati wa warsha hiyo. |
Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akitoa mwongozo wa kazi za vikundi kwa staili ya aina yake kwa washiriki wa warsha ya siku mbili katika utekelezaji wa Mradi mpya wa SHUGA Redio. |
Pichani juu na chini washiriki akitolea maelezo ya picha aliyoichora ikimaanisha nini wakati wa warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa. |
Post a Comment