Nguvu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuzuia wimbi la wanachama wake kutangaza nia ya ‘kumrithi’ Rais Jakaya Kikwete, wakati akiwa bado madarakani, zinaonekana kufifia.

Baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kufikia hatua hiyo, Balozi Ali Abeid Amani Karume ambaye ni mtoto wa pili wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amezungumza na NIPASHE Jumamosi mjini hapa, na kusema ameshajiandaa kuiomba CCM impitishe kuwania kiti hicho kwa sababu ana uwezo na sifa zinazostahili.

“Kweli nategemea kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,”
 alisema Balozi Karume.

Kwa mara ya pili kwa Balozi Karume ambaye ni kaka wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid
Karume, aliomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kuwania nafasi mwaka 2005, lakini hakufanikiwa.

Pia wakati kaka yake, Amani Abeid Karume, akistaafu mwaka 2010, Balozi Karume alijitokeza kutaka kuwania Urais wa Zanzibar mwaka 2010, lakini nafasi hiyo ikachukuliwa na Rais wa sasa, Dk Ali Mohamed Shein.

Akijielekeza katika kuitambua fursa hiyo, Balozi Karume, alisema kuna uwezekano kwa mgombea Urais kupitia CCM kwa Uchaguzi Mkuu ujao, akatokea Zanzibar.

Alisema, kutokana na ‘utabiri’ wake huo, miongoni mwa wana-CCM watano (akiwamo yeye) waliotangaza nia ya kuwania Urais wa Zanzibar 2010, atapewa nafasi hiyo.

Balozi Karume alisema kuwa hakuna kitu kigumu duniani kama kujipima mwenyewe, lakini watu aliozungumza nao (hakuwataja) wamemwambia anafaa kugombea na jambo hilo limempa faraja ya kutangaza nia.

Alisema hana nia ya kugombea Urais wa Zanzibar, kwani angependa nafasi hiyo aendelee nayo rais wa sasa, Dk Ali Mohamed Shein.

HEKAYA ZA UJANA NA UZEE

Balozi Karume, alisema katika suala la Urais hakuna hoja ya ujana wala uzee inayoweza kupata nguvu, bali ni kutimiza vigezo vya kisheria na utaratibu wa CCM unaoainisha sifa 13 na kuwa na afya bora.

Alisema ana imani sifa hizo anazo, hivyo hana pingamizi lolote kuhusu `safari ya kueleka Ikulu’ ya jijini Dar es Salaam.

Balozi Karume kwa muda mrefu alikuwa akifanya kazi ya ubalozi katika nchi za Ulaya.
 
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.