TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Majeshi
Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda
amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni
mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa
na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa
vizuri.
Kwa mujibu wa
Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi pekee
ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake miongoni mwa majeshi bora duniani.
Chini
ya kichwa cha habari "35 Most Badass Elite Fighting Units from Around
the World" mwandishi, Micky Wren anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora
duniani, yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa
kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi na
yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia
kumaliza uhuni wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo
mkubwa.
Mwandishi anasema kuwa orodha hiyo haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa kijeshi wa kila kikundi.
Vikosi
vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile cha Seal cha Jeshi la Maji la
Marekani, SAS cha Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha Majeshi Maalum
ya Denmark, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Kikosi cha MARSOC, Majeshi
Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za usoni zisizoweza kuingiliwa
na risasi na Kikosi cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya Ireland.
Vingine
ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Ugaidi cha
JTF2 cha Canada, Majeshi Maalum ya Uholanzi, Kikosi cha SBS, Majeshi
Maalum ya Jamhuri ya Korea, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Majeshi Maalum
ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha Norway, Canadian Joint Response Unit cha
Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi cha French Commando Marine,
Majeshi Maalum ya New Zealand, Kikosi cha Norwegian Armed Forces Special
Command na Kikosi cha Polish Grom cha Poland.
Vingine
ni Kikosi cha US Army Special Forces Sniper with Remington Modular
Sniper Rifle, Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi Maalum ya Indonesia,
Majeshi Maalum ya Romania, Kikosi cha SASR cha Australia, Kikosi cha KSK
cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani, Majeshi Maalum ya Israel -
Shayetet 13, Majeshi Maalum ya Urusi - Spetsnaz, Majeshi Maalum ya
Austria - Jagdkommando, Majeshi Maalum ya Iraq, Majeshi Maalum ya
Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya Peru.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
3 Julai, 2014
Post a Comment