Mchukueni Theo Walcott na Nipieni pesa talismu £8m na mnipatie na   Raheem.


Kocha Arsene Wenger ametanabaisha ya kuwa yuko tayari kumwachia Winga wake Theo Walcott aliyebakiza muda mchache kumalizika kwa mkataba wake na kukiwa hakuna maafikiano yaliofikiwa juu ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya amesema ni jambo zuri kubaki na wachezaji wako bora lakini ikiwa italazimika kumwuza Walcott basi ni vizuri pia kumbadili na mchezaji mwenye jina kubwa na na mwenye ubora pia.

Arsene Wenger alifikia kutamka maneno hayo yanayoashiria kubadilishana wachezaji  kutokana na mazungumzo yanayoendelea takribani miezi kadhaa sasa baina yao na  ya winga huyo wa kiingereza, Theo mwenye miaka 23. Kwa jinsi inavyoneka ni kwamba Wenger hayuko tayari kutoa mshahara unaokadiriwa kufikia £90,000 kwa wiki.

Kulingana na mkataba wa Theo Walcott atakuwa huru kuongea na timu yeyote itakayomuhitaji kuanzia mwezi Januari na wakati huo huo kinda wa Liverpool Raheem Sterling mwenye miaka 17  amebakiza miezi 18 katika mkataba wake na yuko kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na timu yake.Itakumbukwa pia kocha wa Livepool Brendani Rodger anamuhusudu sana Theo Walcott hivyo kutoa mwanya kwa timu zote mbili kukaa mezani na kujadili mustakabali wa wachezaji wao hao wawili.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.