NCHI ya Uruguay yenye raia takribani milioni 4, inatajwa kuwa na bahati ya kuwa na Rais asiye na chembe ya tamaa. Hana makuu, kiasi
kwamba anatajwa kuwa ndiye Rais masikini zaidi kuwahi kutokea duniani.

Huyu si mwingine, bali ni Jose Mujica, Rais wa sasa wa Uruguay ambaye pia ni Rais wa 40 wa nchi hiyo. Tangu aingie madarakani Machi mosi
mwaka 2010, amekuwa akionekana kuwa kiongozi wa tofauti kabisa, tofauti na waliomtangulia. 
Raisi wa Uruguay, Jose Mujica
 
 
 Mathalan, baada ya kufanikiwa kuishika nchini, hakuwa na tamaa ya kukimbilia Ikulu, yeye alichokifanya ni kuamua kuishi katika makazi
yake yaleyale, katika nyumba ya mkewe iliyoko shambani, nje ya Jiji la Montevideo.

Kwa ujumla, anapenda maisha ya kawaida, maisha ya kuwahurumia wengine na kujitahidi kuonesha kwa vitendo.

Ni vigumu kuamini, licha ya kuwa ni Rais wa nchi, amejishusha mno kiasi cha mara kadhaa kuonekana akijichanganya na raia wake katika
shughuli za ujenzi wa taifa, ikiwamo ujenzi wa barabara, kulima mashamba ya mfano.

Na wakati mwingine, anapougua huwahi kupanga mstari ili kuonana na daktari, akichelewa anapanga mstari kusubiri zamu yake.

Ni Rais pekee ambaye ameamua kutoa mshahara wake kwa zaidi ya asilima 90 kugawana na watu masikini wa nchi yake, kwamba fedha hizo huingizwa
katika vikundi mbalimbali vya maendeleo.

Akiwa amepangiwa na Bunge kupokea dola za Kimarekani 11,000 (sh milioni 17.6 kwa fedha za Tanzania) kwa mwezi, hajawahi kupokea fedha
hizo na ameiamuru Hazina kuzipeleka fedha hizo kwa wananchi masikini.

Yeye hupokea shilingi milioni 3 tu, tena hizi akizitumia kwa ajili ya mafuta ya gari lake alilonunua na mkewe aina ya Volkswagon Beetle
maarufu kama `Mgongo wa Chura’. Gari hilo lenye umri wa miaka 23, ndio utajiri pekee anaojivunia. 
 
 
Mkoko ndani ya Gereji ya Raisi Jose Mujica
 
 
Hana kingine anachokimiliki. Hana akaunti benki, hana nyumba yake binafsi, wala mali nyingine ya aina yoyote aliyojilimbikizia.
Kuhusiana na gari lake lenye thamani ya dola za Kimarekani 1,900 (Sh milioni 3), ambalo analiendesha mwenyewe, anasema:

“Niko mimi na mke wangu, wawili tu, gari kubwa la nini, sina haja nalo, sitaki kuwaibia wananchi, kunichagua tu kuwaongoza ni sifa
pekee, tena kubwa inayokaribia utukufu wa kawaida, sasa zaidi ya hapo nini…

“Nahitaji sana kuwatumikia wananchi wa Uruguay, sio kuwanyonya wala kuwaibia au kuwa mwanya wa kuchuma na kujifurahisha mimi, mke wangu,
watoto wangu na ndugu zangu, sioni haja hiyo na sitaki kuwa mnyonyaji kamwe,” anasema Rais Mujica. Anasisitiza anayafurahia maisha ya
kawaida, hivyo haoni shida kuishi na watu wa kawaida mtaani kwake, kupiga nao porojo na hata kushirikiana katika shughuli za kijamii pale
inapolazimu.

“Nikiwa na akaunti benki, nikiwa na magari makubwa, nitakuwa nakaribisha ushawishi wa kuwa mwizi, kuwaibia wananchi wangu, sitaki
chochote,” anaongeza Rais huyo ambaye hata anapoamua kunyoa nywele zake, hahitaji kinyozi maalumu, bali yeyote anayejua kunyoa anamwita
nyumbani kwake aweze kumnyoa.

Staili ya maisha ya Rais huyo inaonekana pia kumwingia mkewe ambaye pia tofauti na wake wengine wa marais, yeye hajipambi kwa dhahabu,
almasi wala aina nyingine ya vito vya thamani.

Anashirikiana na mumewe katika shamba lao la maua katika makazi yao, huku Rais Mujica wakati mwingine akifanya usafi wa nyumba na hata
kumwagilia maua. Hayo ndiyo maisha ya Jose Mujica, Rais wa 40 wa Uruguay ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 77, lakini licha ya
kupigania mno kuingia Ikulu, ameonesha kutokuwa na kiu ya utajiri, hataki kujikweza na wala kuonekana ni tofauti na watu wengine.

Ndiyo maana ameonekana kuwa Rais wa ajabu, akitajwa pengine kuwa ndiye asiye na makuu na masikini kuliko wote duniani. Hata vaa yake ni ya
kawaida, mara nyingi akiingia ofisini na mavazi ya kawaida, lakini mara moja moja tu, akivalia suti na tai hasa anapokuwa na ugeni mzito.

Angalau Makamu wake, Danilo Astori anaonekana na `ufisadi’ kidogo, kwani ana nyumba yenye thamani ya dola 250,000 (Sh milioni 400) na
gari kama la milioni 30 hivi. Je, kuna wengine wenye staili ya maisha ya Rais Mujica? Yawezekana, lakini kwa sasa imeonekana hakuna kama
Mujica.

Rais Mujica akiteremka ndani ya mkoko wake































































Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.