Habari imeandikwa na Happiness Katabazi
KIONGOZI wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Mukadam Abdal Swalehe (45), jana alijikuta akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akiunganishwa katika kesi ya jinai Na.245/2012 inayomkabili Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Issa Ponda Issa na wenzake 49 wanaokabiliwa na makosa ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. milioni 59 na hivyo kufanya sasa kesi hiyo kufikia idadi ya washtakiwa 51.
Sambamba na hiyo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dkt. Eliezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kumfungua dhamana Mukadamu kwaajili ya maslahi ya taifa chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Mukadam alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa ambaye ndiye anayeisikiliza kesi hiyo tangu mwanzo ambapo wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka aliianza kwa kuieleza mahakama hiyo kuwa upande wa jamhuri unaomba kuifanyia marekebisho hati ya mashitaka ya kesi ya jinai Na. 245/2012 kwasababu imemuongeza mshitakiwa mmoja ambaye ni Mukadam na kwamba Mukadamu anakabiliwa na makosa manne.
Wakili Kweka alidai kuwa kosa la kwanza ni la kuingia kwa nguvu kwenye kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume na kifungu cha 85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Oktoba 12 mwaka huu huko Chang’ombe Markas, wasipokuwa na sababu za msingi waliingia kwa jinai kwenye kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza Ltd, kujimilikisha kiwanja hicho kwa njia ya iloyopelekea uvunjifu wa amani,wizi ambapo baada ya kufamia waliiba vifaa na malighafi ikiwemo nondo, kokoto zenye jumla ya thamani ya Sh. 59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza na kosa la tano ni la uchochezi kinyume na kifungu cha 390 na 35 cah sheria ya Kanuni ya Adhabu, ambalo sasa kosa hili la uchochezi litamkabili Mukadamu na Ponda peke yao kuwa akiwa ni kiongozi wa jumuiya hiyo , Oktoba 12 mwaka huu ,aliwashawishi katika eneo hilo ambapo aliwaamasisha washitakiwa hao watende kosa hilo.
Mshitakiwa huyo alikana mashitaka yote, Wakili Kweka alisema DPP. Feleshi amewasilisha hati ya kufunga dhamana ya Mukadamu na kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika tangu Novemba Mosi mwaka huu na kwamba Novemba 15 mwaka huu, kesi Mukadamu na wenzie 50 watakuja kusomewa maelezo ya awali.
Kwa upande wake hakimu Nongwa alisema makosa yanayomkabili mshtakiwa huyo yana dhamana ila kwakuw DPP-Feleshi amewasilisha hati ya kumfungia dhamana, mahakama imefungwa mikono,haiwezi kutoa dhamana kwasababu sheria iliyotumiwa na DPP kumfungia dhamana mshtakiwa huyo na Ponda zimetungwa na Bunge, mahakama yenye ipo kwaajili ya kuzifuata sheria hizo zilizotungwa na bunge katika kutoa uamuzi hivyo akaamuru mshitakiwa huyo amepelekwe gerezani hadi hadi Novemba 15 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Jana washitakiwa 49 katika kesi hiyo waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana isipokuwa Ponda peke yake ambaye naye dhamana yake imezuiwa na DPP ambapo hivi sasa ni washtakiwa wawili kati ya 49 ndiyo dhamana zao zimefungwa na DPP, yaani Ponda na Mukadam ambao watakuwa wakiendelea kusota gerezani.
---
Mwandishi wa habari ana blogu kupitia: KatabaziHappy.blogspot.com

Post a Comment