NBC yazindua huduma mpya ya BENKI NILIPO kwa njia ya simu za mkononi
BENKI YA TAIFA YA
BIASHARA (NBC) imezindua huduma mpya ya NBC BENKI NILIPO ambapo mteja anaweza
kupata huduma zote za kibenki kupitia simu yake ya mkononi, kompyuta mpakato
kama kulipia bili na huduma zingine popote pale alipo.
Akizungumza kwenye
uzinduzi rasmi wa huduma hizo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa
Benki hiyo, Maria Alina Kimaryo alisema kwamba huduma hizo mpya ni rahisi
kutumia na kurahisisha shughuli za mteja kwa kupitia simu yake ya mkononi na
kompyuta mpakato kwa njia ya intaneti kwa kutoa na kulipa bili zake za luku,
dawasco, dstv na huduma zingine.
“Watu wengi wanaangalia
ni njia gani rahisi ya kuangalia akaunti zao kwa masaa 24 kwa siku kwa kutizama
salio kulipa bili kupitia simu zao za mkononi ili kuweza kuokoa muda na ndipo
benki ya NBC ilipoamua kuja na huduma hizi za kipekee nchini ya BENKI NILIPO
ili kurahisisha shughuli za biashara na za kijamii nchini,” aliongeza
Aliongeza kwamba huduma
hizo mpya zimetengenezwa kwa ajili ya kwenda na wakati wa mazingira ya sasa ya
jamii yenye sayansi na teknolojia ambapo
mteja anaweza kufanya shughuli zote za kibenki bila kulazimika kwenda benki au
kuwa na akaunti na benki ya NBC,
Kimaryo alisema kwamba
ndani ya huduma hiyo mteja anaweza kupata taarifa za akaunti yake, kuhamisha
fedha kwenda kwenye akaunti yake mwenyewe na akaunti nyingine za NBC kwa watu
wengine na kuendesha akaunti yake akiwa ndani au nje ya nchi.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Kitengo cha Njia Mbadala za Kibenki, Raymond Mutagahywa alifafanua kwamba
benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora na bunifu kwa ajili ya wateja wao huku
wakienda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kuboresha huduma za
kibenki nchini.
Alisema kwamba uzinduzi
wa huduma hiyo mpya nchini ni kiashiria tosha kwamba benki hiyo imejipanga
kuendelea kutoa huduma na bidhaa bora kabisa za kibenki hapa nchini na
kuwarahisishia watanzania kwenye huduma za kibenki nchini.
Mutagahywa aliongeza
kwamba kupitia huduma hiyo ya kipekee nchini wateja wa benki hiyo wanaweza
kutuma fedha kwa wapendwa wao ambao pia watakuwa hawana akaunti na benki hiyo
na wateja wa NBC wanaweza pia kuweka fedha kwenye ATMs mahali popote.
Meneja Mahusino wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akiweka mambo sawa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo. |
Add caption |
Baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini ar es Salaam le |