Chuo cha BBC cha Uandishi wa habari chafungua tovuti ya Kiswahili kwa waandishi duniani
Chuo
cha BBC cha Uandishi wa Habari, (BBC Academy, College of Journalism) chafungua
upya tovuti ya Kiswahili kwa ajili ya waandishi wa habari duniani kote.
Chuo
cha BBC cha Uandishi wa Habari kimeanzisha upya tovuti ya Kiswahili katika
mfumo (mtindo) mpya na maswala mapya.
Tovuti
yenyewe inaweza kupatikana kwenye simu ya mkononi, tabiti (tablet) na komputa
kubwa.
Lengo
la tovuti ya Kiswahili ni kuonesha mtindo wa uandishi katika idhaa za lugha
mbali-mbali zinazotangaza katika Idhaa Kuu ya Dunia ya BBC, na ni sehemu ya
jukumu la BBC la kuhudumia jamii na kusambaza ujuzi wake ili kunufaisha
waandishi wa habari wa Kiswahili dunia nzima.
Ali
Saleh, Mhariri wa Idhaa ya Kiswahili:
"Baada
ya serikali za Afrika Mashariki kuruhusu vyombo vingi vya habari binafsi
kuanzishwa, vinatoa ushindani mkubwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa.
Ingawa vyombo hivyo vimestawi na kuzidi kukua, vyombo vinavyojitegemea
vinakabiliwa na tishio katika nchi kadha, ambako waandishi wa habari wamekimbia
kwa sababu ya kulengwa kwa mashambulio na mashtaka. Serikali katika nchi ambako
BBC inasikika zinatayarisha sheria kali kupunguza uhuru wa kujieleza, haki ya
kutofichua chanzo cha taarifa, na kuwafunga waandishi wa habari kwa yale
waliyotangaza."
Tovuti
ina maeneo matatu muhimu, ufundi wa uandishi, lugha ya Kiswahili, na maadili ya
BBC.
Kupitia
sehemu hii ufundiutapata ushauri kuhusu televisheni, redio na mtandao,
utangazaji, uandishi, mitandao ya jamii na mengi mengineyo.
Katika
sehemu hii wahariri na waandishi wa BBC wanaeleza namna ya kutangaza na
kuandika taarifa za televisheni na jinsi ya kuandika ripoti kuhusu michezo.
Tovuti inatoa mwongozo jinsi ya kuthibitisha habari zilizoko kwenye mitandao ya
jamii.
Katika
sehemu yavigezo, kuna ushauri kuhusu msimamo wa kutopendelea upande wowote,
ukweli, uhuru, maslahi ya jamii, uwajibikaji na sheria.
Lakini
msingi wa kila tovuti ni lugha. Sehemu yalugha inatoa ushauri kuhusu lugha
isiyopendelea upande wowote, lugha sahihi, tahajia, ufupisho, majina ya kigeni
na ufundi wa kutafsiri na mengineyo.
Sehemu
ya lugha ya tovuti ina vielelezo vilivyotengenezwa maalumu kulingana na
utamaduni wa Kiswahili. Juhudi zimefanywa kuelezea sehemu hii kwa picha
zinazoonesha Idhaa iliyohusika ya BBC pamoja na wasikilizaji na watazamaji.
Pamoja
na tovuti ya Kiswahili, Chuo cha Uandishi wa Habari cha BBC, (College of
Journalism) piya kinaanzisha lugha tatu nyengine,Burmese,Pashto naVietnamese.
Tovuti hizo nne zinafanya jumla ya tovuti za chuo cha BBC zilizoanzishwa upya
kufikia 11.
Katika
miaka mitano iliyopita BBC College of Journalism, imeanzisha jumla ya tovuti 27
katika lugha tofauti.
Unaweza
kusoma tovuti za BBC College of Journalism bila ya kutozwa pesa kokote uliko
duniani.
KATIKA
miaka mitano iliyopita BBC College of Journalism, imeanzisha jumla ya tovuti 27
katika l
ugha tofauti. Unaweza kusoma tovuti za BBC College of Journalism bila
ya kutozwa pesa kokote uliko duniani.
Chanzo:BBC
Swahili