AWAOMBA MAPOROMOTA KUWAPA NAFASI KUBWA WASANII WA TANZANIA!
ATAKIWA KUELEZA KWA NINI ? NGOMA AFRICA BAND IMEKUWA TISHIO !
Mwanamuziki
Ebrahim Makunja a.k.a Kamanda Ras Makunja kiongozi mwanzilishi wa bendi maarufu
Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni ya kule Ujerumani,juzi kati Kamanda Ras
Makunja aliwekwa kiti moto au kigoda cha moto na kituo cha TV cha Offener
Channel ya Ujerumani. mwengozaji wa kipindi katika mahojiano hayo Bw.Fischer
alimkutanisha Kamanda Ras Makunja na wataalam na wadau wa muziki wa kimataifa.
Akikaribishwa
katika kipindi hicho mwanamuziki Ras Makunja ametajwa kuwa jamii ya ujerumani
inauthamini na kuukubali mchango mchango wake wa kutumia muziki katika kutokomeza
ubaguzi,historia imemtaja Kamanda Ras Makunja na kikosi kazi Ngoma Africa band
kuwa kuanzia mwaka 1993 alikubali kuzunguka ujerumani nzima kufanya maonyesho
ya "WE ARE ONE" onyesho liliofanikiwa kuwaunganisha wageni na wenyeji
kazi ambayo haikuwa rahisi lakini ilifanikiwa.
Lakini pia wadau wa muziki na
mtangazaji walitaka kujua inakuaje ? kwa muda wa miaka 21 Ngoma Africa band
inadumu na kuendelea kuwanasa washabiki kwa wingi ??
Kamanda
Ras Makunja akijibu swali hilo japokuwa alionekana si wakutaka kuweka hadharani
kila mbinu,lakini alifunguka kwa kusema kuwa muziki unachezeka lakini pamoja na
kuchezeka pia wanamuziki wa bendi ya Ngoma Africa band ni watumishi wa
washabiki na wadau wa muziki kwa maana hii bendi inamilikiwa na washabiki na
wadau ambao wao ndio wanayoitangaza. Sisi tuna vyombo vya muziki tu.Mimi
naongoza bendi tu lakini wamiliki ni washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa band
, bandi hii ni sauti ya umma wa kimataifa pia ni sauti ya wasio sikika
"Voice of speachless" ambayo inasikika kimataifa Ras Makunja alisema.
RAS MAKUNJA ALIPOITUMIA FURSA KWA
KUWAOMBA MAPOROMOTA KUWAPA NAFASI WASANII WA TANZANIA!! walio nyumbani.
Kama kawaida yake Kamanda Ras
Makunja bila kujisihau wapi anatoka yaani mtanzania aliyekunywa maji ya
bendera! alipoulizwa juu ya vipaji vya wafrika?
Kamanda
Ras Makunja moja kwa moja aliwaomba wadau na maporomota wa kimataifa kuwapa
nafasi kubwa wanasanii waliopo nyumbani Tanzania kuja kushiriki maonyesho ya
kimataifa, Ras Makunja aliwaomba na kuwashawishi maporomota na wadau hao kuwa
nchi ya Tanzania ina utajiri wa maelfu ya wasanii wenye vipaji vya ajabu
wakiwemo wanamuziki,watengenezaji wasanaa za mikono wanawake kwa
wanaume,wacheza maigizo,sarakasi,wachoraji,nendeni Tanzania mkaonane nao
,wapeni nafasi wasanii hawa muone jinsi watakavyo kuja kufanya sanaa ambazo
hapa ulaya ni adimu sana .
Ninawaombeni nendeni Tanzania na
mkitaka msaada wangu wa kuwaelekeza mimi nipo Tayari - Kamanda Ras Makunja
alimalizia kwa kuwaomba wadau na maporomota.
Kamanda huyu wa Ngoma Africa Band
Ras Makunja alionekana kutumia fulsa kwa
kuwapigania wasanii wa nyumbani ili wapate nafasi zaidi ya kimataifa.
Kamanda Ras Makunja akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuhojiwa |
Post a Comment