Watu wasiofahamika, usiku wa kuamkia jana wameandika maneno kwenye kuta ikiwamo ukuta wa Kampuni ya Bakhressa katika maeneo ya TAZARA wakidhihaki Katiba Inayopendezwa kwa kutaka ipigwe kura ya hapana sanjari na kumshutumu aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta.


Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema inafuatilia kubaini watu wanaoandika maneno ya uchochezi kwenye kuta na kwamba wakigundulika watashitakiwa mahakamani kwa uchochezi na uvunjifu wa amani.

Kamanda wa Polisi katika hiyo Maalumu, Suleiman Kova alisema kwa kutoa maoni kwenye kuta hayatakuwa na thamani, kwani hakuna atakayefanyia kazi. Alishauri jamii kutumia njia muafaka ya kufikisha mawazo yao.

Wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Bakhressa walilazimika kuyafuta kwa kupaka rangi upya kwenye ukuta huo baada ya uongozi kupata taarifa ya kuwepo maandishi hayo.

Hivi karibuni, iliripotiwa kwamba mkoani Dodoma, maandishi kama hayo yalikutwa katika ukuta wa ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.