SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Moblog inaripoti.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano
wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na
kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja
ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati
ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati
ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo
tumekataa,” amesema Balozi Mushy
Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na
wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia
moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka
msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa
maofisa wa wizara ya mambo ya nje pamoja na waziri husika kukataa shinikizo la
kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo.
Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa
kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira,
umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.
Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga
na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha,
historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya
mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru
na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya
millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara
hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi
za mwafrika,”aliongeza
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi
kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo
vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani
nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika
malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa
serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii
baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa
asilimia 85.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona
ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa
nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya
Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima
yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana
kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke
mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa
kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
Mdau mmojawapo akichangia mada yake |
Post a Comment