Nakala ya makubaliano ya vyama vinavyounda UKAWA
Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CUF uliohudhuriwa na wafuasi wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). |
Pichani ni viongozi wa juu wa vyama vinne vya siasa nchini Tanzania
vilivyoingia makubaliano ya ushirikiano wa shughuli mbalimbali za siasa
Oktoba 26, 2014.
Miongoni mwa mambo hayo ni kusimamisha wagombea wa pamoja katika
uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani,
Wawakilishi na Rais katika uchaguzi ujao.
Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Viongozi wa Ukawa wakitia saini hati ya ushirikiano wa vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD. Kutoka kushoto Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbati, Mwenyekiti Wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freman Mbowe na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kushoto) akiwaongoza wananchi kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mkutano wa ushirikiano wa vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD. Kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
Mwenyekiti wa NLD, Dk. Emmanuel Makaidi akitoa hotuba yake katika mkutano wa UKAWA.
Makatibu wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mfuasi wa Chama cha Wananchi CUF akiomba dua kabla ya kuanza kwa mkutano wa UKAWA.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.
Mwakilishi wa Mjimkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu akihutubia katika mkutano wa UKAWA.
Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na UKAWA.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbroad Slaa akihutubia katika mkutano wa UKAWA. Pembeni yake ni kiongozi wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalim.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akihutubia katika mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika viwanja vya Jangwani.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa UKAWA.
Mwanasheria wa Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA) ,Tundu Lissu akionyesha Katiba inayopendekezwa kwa wananchi.
Umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.
Viongozi hao wakishangilia kuzaliwa kwa ushirikiano huo huku makatibu wao wakiwa wameketi.
Wafuasi, wanachama, wa vyama vya siasa vinavyounda ukawa wakifuatilia
mkutano huo ambao ulianza kwa kuimba wimbo wa Taifa huku wanachama hao
wakiwa wamekaa jambo ambalo lilielezwa na viongozi wao kuwa uzalendo ni
ndani ya moyo.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiagana na wananchi waliohudhuria mkutano wa UKAWA.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akisalimia na Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiagana na wananchi waliohudhuria mkutano wa UKAWA.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akisalimia na Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba.
Post a Comment