Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa shindano la Big Brother HOTSHOTS msimu wa tisa iliyoandaliwa maalum kwa wadau wa DStv na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Dar es Salaam Serena |
Shindano linalopendwa
na wengi barani Afrika, maarufu la Big Brother Afrika ambalo kwa
mwaka huu ni la msimu wa 9 likijulikana kama Big Brother Hotshot lililoanza
usiku wa kuamkia leo Tanzania imeng’ara hasa kwa washiriki wake kufanya vizuri katika
muonekano wa awali sambamba na shoo iliyopigwa na mwanamuziki Nasseb Abdul
‘Diamond’ aliyeteka umati uliohudhuria uzinduzi huo.
Halfa hiyo ya masaa
mawili ambayo imeweza kushuhudia washiriki 26, imekuwa gumzo pale
washiriki wanaoiwakilisha Tanzania msimu huu wa 9, Laveda na Idriss wakifanya
kweli katika utambulisho wao huku mwanamuziki Diamond akikonga vilivyo na wimbo
wake wa ‘My Number One’.
Tanzania imekuwa na
bahati ya kipekee kwa mshiriki wake huyo, Laveda ambapo aliteka umati mkubwa
kwa kuonesha uhodari wake wa kupuliza “Saxophone”, hali iliyopelekea kupigiwa
kura nyingi huku akishangiliwa kwa shangwe muda wote.
Kura hizo alizopigiwa
Laveda na kuwa juu ya washiriki wote 26, pia zimemfanya awe Mkuu wa jumba hilo
‘Head of the House’ mpaka hapo itakapoamuliwa na Biggy. Kura alizopigiwa Laveda
ni 85.0 huku mshiriki wa Kenya, Sabina akipata kura 78.3, ambaye yeye
alionyesha uwezo wake wa kuchekesha kwa kutumia maneno.
Kwa upande wa mshiriki
mwingine wa Tanzania, Idriss naye aliweza kukonga nyoyo za wageni wa jumba hilo
waliofurika kwenye uzinduzi ambapo yeye aliweza kucheza kwa ustadi wimbo
maalum. Uchezaji wake na mavazi aliyoyavaa yaliweza kuwa kivutio kikubwa huku
akishangiliwa muda wote, ambapo aliweza kupigiwa kura na kupata alama zaidi ya
60.
Mpaka hatua ya mwisho,
muongozaji wa BBA, IK alieleza kuwa, Tanzania imekuwa kinara kwa washiriki wake
hao hasa baada ya kuonyesha kipaji cha hali ya juu.
Shindano hilo la kila
mwaka, linaloandaliwa na kampuni ya Multchoice, linashirikisha washiriki kutoka
nchi 14 za bara la Afrika na mshindi anatarajiwa kuondoka na kitita cha dola
300,000, Baadhi ya nchi hizo zilizotoa washiriki ni pamoja na Angola, Botswana,
Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Kenya, Malawi, Zambia, Namibia, Ghana,
Nigeria, na Zimbabwe.
Shindano hilo
lililoanza rasmi 2003, Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwa washiriki wake,
akiwemo Mwisho Mwampamba pamoja na Richard Bezuidenhout ambao waliweza kung’ara
ikiwemo Richard aliyewahi kutwaa taji hilo.
Kwa upande wa Tanzania,
shangwe zilitawala kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakishuhudia uzinduzi huo
moja kwa moja kwenye halfa maalum iliyoandaliwa na DStv Tanzania ndani ya
hoteli ya Serena, ambapo walipongeza huku wakiahidi kuwapa sapoti kubwa
washiriki wao.
Baadhi ya wadau
hao wakiwemo watu maarufu walioungana na wandishi wa habari, team ya DStv
Tanzania na wateja wa DStv akiwemo Aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika
Shindano la msimu wa 7 wa Big Brother Stargame 2012 Julio Batalia.
Walisema washiriki hao
wameonyesa mwanzo mzuri hivyo kila mtanzania anatakiwa kujivunia na hata
kuwapa sapoti.
Mwandishi wa gazeti la The African, Sidi Mgumia (katikati) akipata ukodak na wadau |
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam, Florenso Kirambata, Blogger Seif Kabelele, Blogger Jestina George Meru #Diaspora na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu. |
Wageni waalikwa katika picha |
Wageni waalikwa wakinywa na kubadilishana mawazo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Big Brother HOTSHOTS uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Serena Dar es Salaam |
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu akibadilishana mawazo na Aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la msimu wa 7 wa Big Brother Stargame 2012 Julio Batalia (kulia) wakati wa sherehe za uzinduzi wa shindano la Big Brother HOTSHOTS lilizinduliwa usiku wa kuamkia leo na kuwapa fursa wadau wa DStv na waandishi wa habari kushuhudia Live kwenye big screen kubwa ndani ya hoteli ya Dar es Salaam Serena |
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu katika picha na mshiriki huyo |
Juu na chini ni Baadhi ya waliohudhuria hafla hiyo |
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, akishow love na msanii wa muziki nchini aliyewahi kutumbuiza kwenye moja ya shindano la Big Brother Africa C.P ak.a CPWAA |
Blogger Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog akibadilishana mawazo na Mike Mushi wa Jamii Forums (kushoto) kwenye hafla hiyo iliyofana ndani ya hoteli ya Dar es Salaam Serena usiku wa kuamkia leo |
Post a Comment