TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Lusekelo Mwaseba kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
IMG_0527
Bwana Lusekelo Mwaseba pichani

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mwaseba alikuwa Kamishna wa Uchunguzi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2014.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.